Loading...
title : Kampuni 3 Kuuza Tanzanite katika Mnada Wa Mirerani
link : Kampuni 3 Kuuza Tanzanite katika Mnada Wa Mirerani
Kampuni 3 Kuuza Tanzanite katika Mnada Wa Mirerani
Na Zuena Msuya, Manyara.
Kampuni tatu za uchimbaji madini ya Tanzanite zimejitokeza kuuza madini hayo katika mnada wa tatu wa madini ya Tanzanite unaofanyika katika mji mdogo wa Mirerani wilayani Simanjiro mkoani Manyara.
Mshindi wa mnada huo atatangazwa Desemba 21 katika eneo la Naisinyai lililoko kwenye mji mdogo wa Mirerani.Kamishna wa Madini, Mhandisi Benjamin Mchwampaka amezitaja kampuni hizo kuwa ni Tanzaniteone yenye ubia na Shirika la Madini Tanzania( STAMICO), Tanzanite Afrika na Classic Gems.
Akizungumzia mnada huo, Kamishna Mchwampaka alisema kuwa utaratibu wa kufanya Mnada wa Tanzanite ni jitihada za Serikali za kudhibiti utoroshwaji wa madini hayo nje nchi na pia kuwasaidia wachimbaji na wafanyabiashara wazalendo kuuza madini yao kwa bei ya ushindani inayoendana na soko la dunia.
Mchwampaka alifafanua kuwa, mnunuzi atakayefanikiwa kununua madini katika mnada huo ni yule tu atakayetoa bei ya juu ambayo imefikia au kuvuka bei inayotokana na Wathamini wa Serikali (Reserve Price).
Katibu Mkuu Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila( katikati) akielezwa jambo na Vikosi vya ulinzi na usalama, katika eneo linalotumika kufanyia mnada wa Madini ya Tanzanite katika eneo la Naisinyai lililoko kwenye mji mdogo wa Mirerani.
Katibu Mkuu Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila( katikati) akiangalia mapambo na vitu mbalimbali vinavyotengezwa na Kituo cha Uongezaji thamani Madini ya vito na Miamba( TGC),kilichopo mkoani Arusha, wakati Mnada wa Madini ya Tanzanite unaofanyika katika Mji mdogo wa Mirerani mkoani Manyara.
Wanunuzi kutoka mataifa mbalimbali wakifanya uthamini wa Madini ya Tanzanite kabla ya mnada kufanyika katika eneo la Naisinyai lililoko kwenye mji mdogo wa Mirerani.
Hivyo makala Kampuni 3 Kuuza Tanzanite katika Mnada Wa Mirerani
yaani makala yote Kampuni 3 Kuuza Tanzanite katika Mnada Wa Mirerani Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Kampuni 3 Kuuza Tanzanite katika Mnada Wa Mirerani mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/12/kampuni-3-kuuza-tanzanite-katika-mnada.html
0 Response to "Kampuni 3 Kuuza Tanzanite katika Mnada Wa Mirerani"
Post a Comment