Loading...
title : SHUWASA,POLISI WATEKETEZA VIFAA VINAVYOTUMIKA KUHARIBU VYANZO VYA MAJI BWAWA LA NING'WA SHINYANGA
link : SHUWASA,POLISI WATEKETEZA VIFAA VINAVYOTUMIKA KUHARIBU VYANZO VYA MAJI BWAWA LA NING'WA SHINYANGA
SHUWASA,POLISI WATEKETEZA VIFAA VINAVYOTUMIKA KUHARIBU VYANZO VYA MAJI BWAWA LA NING'WA SHINYANGA
Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira mjini Shinyanga (SHUWASA) kwa kushirikiana na jeshi la polisi wilaya ya Shinyanga wameendesha zoezi la kuteketeza vifaa vinavyotumika kuharibu vyanzo vya maji katika bwawa la Ning’wa.
Miongoni mwa vifaa vilivyoteketezwa kwa moto ni nyavu za kuvulia samaki,mitumbwi na vibanda vinavyotumiwa na wavuvi kujihifadhi karibu na bwawa hilo.Zoezi hilo limefanyika leo Jumanne Desemba 19,2017 katika bwawa hilo lenye mita za ujazo milioni 10.9 linalopatikana katika kata za Old Shinyanga,Chibe na Pandagichiza zilizopo katika wilaya ya Shinyanga.
Akizungumza wakati wa zoezi hilo,Mkurugenzi wa SHUWASA,Injinia Sylivester Mahole alisema lengo la oparesheni hiyo aliyodai ni endelevu, ni kuhifadhi vyanzo vya maji kwani bwawa hilo ni moja vya vyanzo muhimu vya maji vya mamlaka hiyo ukiachilia mbali Ziwa Victoria.
“Tumeteketeza kwa moto vifaa vilivyokuwa vinatumika kwa shughuli za uvuvi katika bwawa hili ikiwemo mitumbwi,nyavu na vibanda vilivyokuwa vinatumiwa na wavuvi,tunataka waache mara moja kufanya uvuvi hapa kwani wanaharibu vyanzo vya maji”,alieleza Injinia Mahole.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira mjini Shinyanga (SHUWASA),Injinia Sylivester Mahole akielezea lengo la kuendesha oparesheni ya kuteketeza kwa moto vifaa vinavyotumiwa na wananchi kuharibu vyanzo vya maji katika bwawa la Ning'wa.Kulia ni mwandishi wa habari wa Radio Faraja na DW,Veronica Natalis - Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira mjini Shinyanga (SHUWASA),Injinia Sylivester Mahole akionesha mifugo katika bwawa la Ning'wa .
Askari polisi akishirikiana na mwananchi kuondoa mtego wa samaki katika bwawa la Ning'wa
Askari polisi akimwaga mafuta kwa ajili ya kuchoma moto nyavu zinazotumika kuvua samaki katika bwawa la Ning'wa
Moto ukiteketeza nyavu .
Hivyo makala SHUWASA,POLISI WATEKETEZA VIFAA VINAVYOTUMIKA KUHARIBU VYANZO VYA MAJI BWAWA LA NING'WA SHINYANGA
yaani makala yote SHUWASA,POLISI WATEKETEZA VIFAA VINAVYOTUMIKA KUHARIBU VYANZO VYA MAJI BWAWA LA NING'WA SHINYANGA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala SHUWASA,POLISI WATEKETEZA VIFAA VINAVYOTUMIKA KUHARIBU VYANZO VYA MAJI BWAWA LA NING'WA SHINYANGA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/12/shuwasapolisi-wateketeza-vifaa.html
0 Response to "SHUWASA,POLISI WATEKETEZA VIFAA VINAVYOTUMIKA KUHARIBU VYANZO VYA MAJI BWAWA LA NING'WA SHINYANGA"
Post a Comment