Loading...
title : KIGOMA UJIJI KUPITIWA UPYA MIKATABA YA UPANGISHAJI
link : KIGOMA UJIJI KUPITIWA UPYA MIKATABA YA UPANGISHAJI
KIGOMA UJIJI KUPITIWA UPYA MIKATABA YA UPANGISHAJI
HALMASHAURI ya Manispaa ya Kigoma Ujiji imetangaza kupitia upya mikataba ya upangishaji kwenye masoko yake, ili kuwawezesha wafanyabiashara wanaoendesha biashara kwenye masoko hayo kuwa ndiyo wapangaji kwenye vibanda vilivyopo kwenye masoko hayo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Uchumi, Elimu na Afya Yunus Ruhonvya alitangaza hayo kwenye kikao cha kawaida cha robo mwaka cha Baraza la Madiwani la halmashauri hiyo. Alisema halmashauri inakusudia kuwaondoa kwenye masoko yake watu wanaowapangisha kiasi kikubwa cha fedha wafanyabiashara, jambo ambalo linawaumiza wafanyabiashara hao kiuchumi.
Akijibu malalamiko ya madiwani wa halmashauri waliotaka kujua hatua ambazo halmashauri inachukua kutokana na kusuasua kulipwa kwa kodi mpya ya pango ya Sh 50,000 kutoka Sh 15,000 ya awali.
Katika hilo alisema kuwa wapo watu ambao wanamiliki vibanda baada ya kuchukua vibanda kwa kuandikishiana mkataba na halmashauri lakini watu hao hawafanyi biashara kwenye vibanda hivyo, badala yake huvikodisha kwa wafanyabiashara kwa kodi ya Sh 200,000. Awali Diwani wa kata ya Businde, Masudi Omari alisema bado mapato yanayopatikana katika ukodishaji wa vibanda na makusanyo kutoka kwenye masoko hayatoshelezi, hivyo kushindwa kuifanya halmashauri kufikia lengo la ukusanyaji
Hivyo makala KIGOMA UJIJI KUPITIWA UPYA MIKATABA YA UPANGISHAJI
yaani makala yote KIGOMA UJIJI KUPITIWA UPYA MIKATABA YA UPANGISHAJI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala KIGOMA UJIJI KUPITIWA UPYA MIKATABA YA UPANGISHAJI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/12/kigoma-ujiji-kupitiwa-upya-mikataba-ya.html
0 Response to "KIGOMA UJIJI KUPITIWA UPYA MIKATABA YA UPANGISHAJI"
Post a Comment