Loading...

MAASKOFU WAFUNGUKA, WATOA YA MOYONI

Loading...
MAASKOFU WAFUNGUKA, WATOA YA MOYONI - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MAASKOFU WAFUNGUKA, WATOA YA MOYONI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MAASKOFU WAFUNGUKA, WATOA YA MOYONI
link : MAASKOFU WAFUNGUKA, WATOA YA MOYONI

soma pia


MAASKOFU WAFUNGUKA, WATOA YA MOYONI

*MMOJA ATAKA WATANZANIA KUACHA KULALAMA VYUMA KUKAZA

Na Said Mwishehe,Blogu ya Jamii

MAASKOFU mbalimbali nchini wameitumia Sikukuu ya Krismasi kuelezea mambo mbalimbali yanayoendelea nchini.

Huku baadhi yao wakimpongeza Rais,Dk.John Magufuli kwa uamuzi wake wa kuachia baadhi ya wafungwa waliokuwa wamehukumiwa kunyongwa na wale wa vifungo vya maisha jela.

Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Zanzibar, Augustine Shao, amempongeza Rais kuwaachia huru wafungwa hao kwani inaonesha wazi anaamini waliopo magerezani wakiwemo vijana wataendelea kujirekebisha na kuwa na tabia njema inayompendeza Mungu na jamii nzima.

Pia amewataka waumini wa Kikristo kujitakasa upya hasa katika Sikukuu ya Krismasi . “Ni vema pia Watanzania kila mmoja wetu akaheshimu mawazo ya mwenzake hata kama yanatofautiana”.


Askofu Pengo ahimiza mema

Askofu Mkuu wa Jimbo Katoliki la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, amesisitiza umuhimu wa Watanzania kutenda matendo mema na kuongozwa na hofu ya Mungu.

Askofu Pengo amesema hayo kwenye Misa ya pili ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo iliyofanyika Kanisa Kuu la Mtakatifu Joseph jijini Dar es Salaam.

Amesema maendeleo hayawezi kuja kama Watanzania wenyewe hawana maadili au hofu ya Mungu.“Kila mmoja wetu awe mwananchi au kiongozi, anapaswa kuwa na hofu ya Mungu itakayomuongoza katika kufanikisha mipango iliyokusudiwa au aliyoikusudia.

“Pia Watanzania wanapaswa kukubali kuongozwa na kuwaombea viongozi wao ili jitihada zinazofanywa zizae matunda mema kwa maendeleo ya nchi yetu na watu wake,” amesema Askofu Pengo.

ASKOFU Amani azungumzia utekaji nyara

Wakati huo huo Askofu wa Jimbo Katoliki Moshi, mkoani Kilimanjaro Isack Amani, amekemea vitendo vya ukatili vikiwamo vya utekaji nyara na mauaji ya kinyama yanayoendelea katika baadhi ya maeneo nchini.

Amesema matukio hayo yanatishia kutoweka kwa amani iliyopiganiwa na waasisi wa Taifa kwa miaka mingi.

Akihubiri kwenye ibada ya Krismasi iliyofanyika Kanisa Kuu la Kristu Mfalme Moshi, Askofu Amani alisema katika kipindi cha muda mfupi kumeibuka matukio yanayohatarisha amani ya nchi yetu.



Hivyo makala MAASKOFU WAFUNGUKA, WATOA YA MOYONI

yaani makala yote MAASKOFU WAFUNGUKA, WATOA YA MOYONI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MAASKOFU WAFUNGUKA, WATOA YA MOYONI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/12/maaskofu-wafunguka-watoa-ya-moyoni.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "MAASKOFU WAFUNGUKA, WATOA YA MOYONI"

Post a Comment

Loading...