Loading...

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Afunga Kongamano la Kiswali la Kimataifa Zanzibar.

Loading...
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Afunga Kongamano la Kiswali la Kimataifa Zanzibar. - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Afunga Kongamano la Kiswali la Kimataifa Zanzibar., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Afunga Kongamano la Kiswali la Kimataifa Zanzibar.
link : Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Afunga Kongamano la Kiswali la Kimataifa Zanzibar.

soma pia


Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Afunga Kongamano la Kiswali la Kimataifa Zanzibar.




Na. Othman Khamis OMPR.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema wakati umefika kwa Wafanyabiashara  wakubwa Nchini kuwekeza katika uchapishaji wa Vitabu vya Kiswahili pamoja na kujenga Maduka makubwa ya kuuzia kazi za Kiswahili kwa vile bidhaa  zinazotokana na lugha hiyo zinauzika.

Alisema  Mwanataaluma au mswahili anayehitaji vitabu  vya Waandishi Mahiri wa Lugha hiyo  wa Zanzibar  kama Profesa Said Ahmed Mohamed, Shafi Adam Shafi, Bwana Msa na wasanii  wengine kama Mohamed Seif  Khatibu kamwe kwa wakati huu anashindwa kuvipata.

Balozi Seif Ali Iddi alisema hayo wakati alipokuwa akilifunga Kongamano la Kimataifa la Siku mbili la Lugha ya Kiswahili lililokuwa likifanyika katika Ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar uliopo Mtaa wa Kikwajuni Mjini Zanzibar.

Alisema ni faraja iliyoje kwa sasa kuona kiasi gani Lugha ya Kiswahili inavyoendelea kupata heshima ya kutambuliwa na kukubaliwa Kimataifa hasa kutokana na upatikanaji wa mwitiko mkubwa wa kuwa na Wataalamu waliobobea katika nyanja mbali mbali.

Balozi Seif aliwataka Wafanyabiashara, Wataalamu pamoja na watumiaji wa Lugha ya Kiswahili ndani na nje ya Nchi kushirikana kwa pamoja katika  kuhakikisha Lugha hiyo inatumika ipasavyo na hasa ikitambulika  wazi kwamba hakuna mtu anayeelewa kila kitu.

“Hakuna Mtaalamu anayejuwa kila kitu. Utamkuta Mtaalamu wa Fasihi Sarufi inampiga chenga au Mtaalamu wa muundo wa L ugha Sarufi inamuendesha kindumbwe ndumbwe ”. Alisema Balozi Seif.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwapongeza waandaaji wa Kongamano hilo la Kimataifa la Kiswahili ambalo limewaweka pamoja Wataalamu wa Kiswahili kutoka Tanzania Bara, Ulaya Marekani baadhi ya Nchini za Bara la Afrika na wenyeji Zanzibar.

Alisema ni kawaida katika mijadala kama hiyo ya Kitaaluma washiriki huchangia kwa kuhoji,kuboresha au kutokubaliana na baadhi ya vipengele vya Hoja mambo ambayo yanapaswa kuigwa na kuzingatiwa na wadau wengine kwani huzidi kukipa uhai zaidi Kiswahili Kitaaluma.

Alieleza kwamba Kongamano hilo la Kiswahili limetoa fursa ya mkusanyiko wa Wataalamu wa Taaluma ya nyanja mbali mbali, kukutana na kubadilishana uzoefu, ujuzi na changamoto wanazokumbana nazo wakiwa kwenye harakati za kukiendeleza Kiswahili.

Balozi Seif alifahamisha kwamba mkusanyiko huo sio tu utaimarisha na kukuza Lugha ya Kiswahili, bali pia utajenga wigo mpana zaidi kwa wanataalamu wa Lugha hiyo Dunia nzima kusaidiana katika kukieneza Kiswahili.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwasisitiza wana kongamano hao wa Lugha ya Kiswahili kuwa hivi sasa ni wakati muwafaka wa kufikiria uandaaji wa Maonyesho ya Kimataifa ya Vitabu vya Kiswahili hasa katika Ukanda wa Afrika Mashariki.

Alisema maonyesho hayo ambayo ingependeza yakafanyika kila baada ya Miaka miwili au zaidi yatasaidia kuongeza kasi ya uchapishaji na pengine usomaji wa kazi mbali mbali zinazotokana na Lugha ya Kiswahili.

Mapema Mwenyekiti wa Baraza la Kiswahili Zanzibar { BAKIZA} Dr. Mohamed Seif  Khatib ameipongeza na kuishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar  kwa kuthamini Lugha ya Kiswahili inayopelekea kutumika katika Taasisi zake  za Umma na Jamii.

Dr. Khatib alisema kitendo hicho kinaendelea kuleta faraja kwa Wana Baraza la Kiswahili Zanzibar na kusisitiza kwamba lazima Lugha hiyo iimarishwe ili iweze kurahisisha Maisha ya Mswahili.

Alifahamisha kwamba Mswahili tokea anazaliwa, anakua na kusoma, anaingia katika harakati za Kimaisha, anafariki kwa kumaliza muda wake wa kuishi anaombewa Dua kwa Lugha ya Kiswahili.

Akimkaribisha Mgeni Rasmi kulifunga Kongamano hilo la kwanza la Kimataifa la Kiswahili Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Mheshimiwa Rashid Ali Juma aliupongeza Uongozi wa Baraza la Kiswahili Zanzibar  kwa juhudi kubwa zilizopelekea kufanyika kwa Kongamano hilo Visiwani Zanzibar.

Mh. Rashid alisema Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Mic hezo itakuwa chachu ya kusimamia yale yote yaliyokusanywa katika Kongamano hilo ili yasaidie kunufaisha Kizazi cha sasa na kijacho.

Waziri wa Habari alisema wakati Zanzibar  ikiendelea kuimarisha  miundombinu ya Sekta ya Utalii Kiswahili ni moja ya kivutio kinachoshawishi wageni wengi kupendelea kutembelea Zanzibar kujifunza Utamaduni wa Visiwa hivi kupitia lugha ya Kiswahili.

Alisema Mataifa mengi Duniani hivi sasa yameshaelewa umuhimu na thamani ya Lugha ya Kiswahili kwa kufundisha Wananchi wao. Hivyo kitendo hicho ni vyema kikatiliwa mkazo katika kuona walimu wa kutosha wa kusomesha lugha hiyo hasa kwa wageni wanapatikana katika dhana nzima wa kuilinda lugha hiyo isipotoshwe.


Hivyo makala Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Afunga Kongamano la Kiswali la Kimataifa Zanzibar.

yaani makala yote Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Afunga Kongamano la Kiswali la Kimataifa Zanzibar. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Afunga Kongamano la Kiswali la Kimataifa Zanzibar. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/12/makamu-wa-pili-wa-rais-wa-zanzibar_22.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Afunga Kongamano la Kiswali la Kimataifa Zanzibar."

Post a Comment

Loading...