Loading...

Mpango wa Malipo kwa Ufanisi waleta Mabadiliko Sekta ya Afya Rufiji

Loading...
Mpango wa Malipo kwa Ufanisi waleta Mabadiliko Sekta ya Afya Rufiji - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Mpango wa Malipo kwa Ufanisi waleta Mabadiliko Sekta ya Afya Rufiji, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Mpango wa Malipo kwa Ufanisi waleta Mabadiliko Sekta ya Afya Rufiji
link : Mpango wa Malipo kwa Ufanisi waleta Mabadiliko Sekta ya Afya Rufiji

soma pia


Mpango wa Malipo kwa Ufanisi waleta Mabadiliko Sekta ya Afya Rufiji


Na.WAMJW-Rufiji.

Utekelezaji wa mpango wa malipo kwa ufanisi(RBF) Wilayani Rufiji umeleta mabadiliko makubwa katika Vituo vya afya na Zahanati kwa uboreshaji wa miundombinu pamoja na upatikanaji wa dawa muhimu

Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu  wakati alipotembelea Kituo cha Afya cha Ikwiriri na Zahanati ya Nyamwage katika ziara yake ya kuangalia utekelezaji unaofanyika kupitia mpango wa malipo kwa ufanisi unaotekelezwa katika mikoa nane nchini

Waziri Ummy alisema mabadiliko hayo katika sekta ya afya yamefanyika katika maeneo ya utoaji huduma,Uongozi na Utawala,Rasilimali watu,Mifumo ya usimamizi wa utoaji taarifa za afya,madawa na teknolojia ya afya ambapo mfumo huo umesaidia maboresho, uwajibikaji,ufanisi na usawa kwani dhana hiyo inamfanya mtoa huduma kulipwa kulingana na matokeo ya kazi yake ambayo amehakikiwa na hivyo kufanya vituo hivyo kuongeza hali ya upatikanaji wa dawa na kuboresha miundombinu ya vituo hivyo

"Tumeanza mpango huu katika mikoa 8,tumefanya tathimini kwenye vituo vya afya na zahanati zote za Mkoa wa Pwani ikiwemo Wilaya ya Rufiji,tukabaini vituo vya afya na zahanati hazikuwa na viwango vya ubora unaotakiwa, tukaona tuwapatie  shilingi milioni 10 kila kituo vilivyokidhi kwa ajili ya kuboresha miundombinu"alisema Waziri ummy.

Hata hivvyo aliipongeza kamati ya afya ya kijiji cha Nyamwage kwa kutumia ipasavyo shilingi milioni 10 kwa kuongeza urefu wa paa na kupaua,kuweka malumaru na kuongeza matundu ya choo pamoja na tundu moja la choo kwa ajili ya walemavu"nikupongeze mganga mfawidhi kwa kuboresha zahanati hii kwakweli unapaswa kupongezwa kwani umefanya vizuri ila badilika lugha chafu kwa wananchi haitakiwi,nakupa mwezi mmoja ila kwa upande huu mwingine umenifurahisa,mnyonge mnyongeni ila haki yake mpeni"

Mpango wa Malipo kwa Ufanisi waleta mabadiliko hayo ikiwemo ujenzi na ukarabati wa choo na jengo hilo,kama jengo lionekanavyo pichani juu na chini Waziri Ummy akikagua choo hicho.

Waziri Ummy Mwalimu akipokea mabango kutoka kwa wananchi yenye jumbe mbalimbali kuhusiana na changamoto za Afya, wakati alipokuwa akitembelea Kituo cha Afya cha Ikwiriri na Zahanati ya Nyamwage katika ziara yake ya kuangalia utekelezaji unaofanyika kupitia mpango wa malipo kwa ufanisi unaotekelezwa katika mikoa nane nchini. 
 Waziri wa Afy,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu  akimwelekeza mmoja wa Wazee waliopata vitambulisho vya Matibabu bure kwa Wazee wakati wa tukio hilo mapema leo Wilayani Rufiji.
  Waziri wa Afy,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu  akimkabidhi mmoja wa Wazee kitambulisho cha Matibabu bure kwa Wazee wakati wa tukio hilo mapema leo Wilayani Rufiji.
  Waziri wa Afy,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu  akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuwakabidhi baadhi ya Wazee vitambulisho vya Matibabu bure kwa Wazee alipokuwa akitembelea Kituo cha Afya cha Ikwiriri na Zahanati ya Nyamwage katika ziara yake ya kuangalia utekelezaji unaofanyika kupitia mpango wa malipo kwa ufanisi unaotekelezwa katika mikoa nane nchini. 



Hivyo makala Mpango wa Malipo kwa Ufanisi waleta Mabadiliko Sekta ya Afya Rufiji

yaani makala yote Mpango wa Malipo kwa Ufanisi waleta Mabadiliko Sekta ya Afya Rufiji Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Mpango wa Malipo kwa Ufanisi waleta Mabadiliko Sekta ya Afya Rufiji mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/12/mpango-wa-malipo-kwa-ufanisi-waleta.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Mpango wa Malipo kwa Ufanisi waleta Mabadiliko Sekta ya Afya Rufiji"

Post a Comment

Loading...