Loading...
title : MWENYE TAARIFA KUPOTEA KWA MWANDISHI WA MWANANCHI ATULETEE-POLISI
link : MWENYE TAARIFA KUPOTEA KWA MWANDISHI WA MWANANCHI ATULETEE-POLISI
MWENYE TAARIFA KUPOTEA KWA MWANDISHI WA MWANANCHI ATULETEE-POLISI
JESHI la Polisi nchini limesema yoyote mwenye taarifa zitakazosaidia kupatikana kwa mwandishi wa habari wa kujitegemea wa Kampuni ya Mwananchi Communication(MCL)mkoani Pwani Azory Gwanda ambaye kwa sasa hajajulikana alipo azipeleke kwenye jeshi hilo ili zifanyiwe kazi.
Kauli hiyo imetolewa Dar es Salaam leo na Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai(DCI)Robert Boaz ambapo amesema wanaendelea na upelelezi kutokana na taarifa walizonazo lakini bado wanaendelea kupokea taarifa,hivyo kwa mtu ambaye atakuwa nazo ni vema akawapelekea.
Amesema hayo wakati anajibu swali la waandishi wa habari waliotaka kujua Polisi wamefikia wapi katika kumtafuta mwandishi huyo.
“Jeshi la Polisi tunaendelea kufanya upepelezi kupitia taarifa tulizonazo ambazo hatuwezi kuzisema, lakini tutoe rai kwa mwenye taarifa zaidi zitakazaotusaidia kwenye upepelezi wetu atuletee.
“Ni mapema mno kusema Gwanda ametekwa au amejiteka, kikubwa tuacheni polisi tuendelee na kazi yetu ya kufuatilia,”amesema.
Ameongeza kuwa jamii isubiri upepelezi utakapikamilika utatoa majibu sahihi na kuan mifano ya matukio ambayo yametokea huko nyuma ambapo jamii iliamini mtu fulani ametekwa kumbe amejiteka mwenyewe. Hivyo waachwe wafuatilie na ukweli utajulikana.
Hivyo makala MWENYE TAARIFA KUPOTEA KWA MWANDISHI WA MWANANCHI ATULETEE-POLISI
yaani makala yote MWENYE TAARIFA KUPOTEA KWA MWANDISHI WA MWANANCHI ATULETEE-POLISI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MWENYE TAARIFA KUPOTEA KWA MWANDISHI WA MWANANCHI ATULETEE-POLISI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/12/mwenye-taarifa-kupotea-kwa-mwandishi-wa.html
0 Response to "MWENYE TAARIFA KUPOTEA KWA MWANDISHI WA MWANANCHI ATULETEE-POLISI"
Post a Comment