Loading...
title : NAIBU WAZIRI NISHATI SUBIRA MGALU AAGIZA REA KUMCHUKULIA HATUA MKANDARASI WA AWAMU YA PILI MKOA WA PWANI
link : NAIBU WAZIRI NISHATI SUBIRA MGALU AAGIZA REA KUMCHUKULIA HATUA MKANDARASI WA AWAMU YA PILI MKOA WA PWANI
NAIBU WAZIRI NISHATI SUBIRA MGALU AAGIZA REA KUMCHUKULIA HATUA MKANDARASI WA AWAMU YA PILI MKOA WA PWANI
Na Zainab Nyamka,Globu ya Jamii.
NAIBU Waziri wa Nishati Subira Mgalu ameagiza mkandarasi wa mradi wa umeme wa Vijijini REA awamu ya pili Kwa Mkoa wa Pwani ambayo ni kampuni ya MBH kuchukuliwa hatua hatua kali za kisheria.
Hatua hiyo imefikia baada ya mkandarasi huyo Kampuni ya MBH kushindwa kutimiza malengo ya mkataba na kuacha baadhi ya maeneo yakiwa hajaweka miundo mbinu ya umeme kama walivyokubaliana awali.
Akitoa maagizo hayo mbele ya wananchi wa Kata ya Ruauke, Naibu Waziri Nishati Subira amewataka REA kuhakikisha suala la mkandarasi huyo linachukuliwa hatua kwani ameweza kuacha maeneo mengi yakiwa hayajakamilika na tayari mkataba wake ukiwa umeshamalizika.
Subira amesema maeneo mbalimbali ya ikiwemo Mkamba, Kisarawe, Kibaha Vijijini, Mkuranga, Kibiti, Kisiju na hata Rufiji kuacha maeneo mengi yakiwa hayajakilimika na mengine akiacha nguzo za umeme zikiwa zimesimama bila kuwekwa nyaya za umeme.
"REA lazima muhakikishe mkandarasi huyu anachukuliwa hatua kali za kisheria kwa kushindwa kufikia malengo kwani kuna maeneo mengi ameshindwa kutimiza malengi tuliyokubaliana na tayari mda wake ukiwa umeisha tayari wa kuweka miundi mbinu ya umeme,'amesema Subira.
Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu akiwasalimia wananchi wa Kijiji cha Uruma kilichopo Delta ya Kusini wakati wa ziara yake ya katika Wilaya ya Kibiti.
Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu akikagua miundo mbinu ya shule ya Mtanga Delta akiwa ameambatana na Mkuu wa Wilaya Kibiti Shaban Kiffu,Mbunge wa Jimbo la Kibiti Seif Ally Ungando, Mkurugenzi wa Wilaya ya Kibiti Alvera Ndabagoye na Mkuu wa Shule ya Sekondari hiyo Humphrey Mwakyambiki.
Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu akizungumza na wananchi wa kijiji cha Muyuyu kata ya Mtunda wakati wa ziara yake ndani ya Wilaya ya Kibiti.
Mkuu wa Wilaya ya Kibiti Shaban Kiffu akizungumza na wananchi wa kijiji cha Uruma kichopo Delta ya Kusini wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu.
Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu akizungumza na wakina mama waliokuwa wamewapeleka watoto wao kupata chanjo katika kituo cha afya kilichopo Kijiji cha Muyuyu wakati wa ziara yake ndani ya Wilaya ya Kibiti.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akikabidhi mifuko ya saruji 50 kwa niaba ya Mbunge wa Jimbo hilo, Seif Ally Ungando kwa diwani wa kata ya Ruauke, Mwarami Mkopi kwa ajili ya ujenzi wa Zahanati ya Nyamatanga wakati wa ziara yake ndani ya wilaya ya Kibiti.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala NAIBU WAZIRI NISHATI SUBIRA MGALU AAGIZA REA KUMCHUKULIA HATUA MKANDARASI WA AWAMU YA PILI MKOA WA PWANI
yaani makala yote NAIBU WAZIRI NISHATI SUBIRA MGALU AAGIZA REA KUMCHUKULIA HATUA MKANDARASI WA AWAMU YA PILI MKOA WA PWANI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala NAIBU WAZIRI NISHATI SUBIRA MGALU AAGIZA REA KUMCHUKULIA HATUA MKANDARASI WA AWAMU YA PILI MKOA WA PWANI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/12/naibu-waziri-nishati-subira-mgalu_28.html
0 Response to "NAIBU WAZIRI NISHATI SUBIRA MGALU AAGIZA REA KUMCHUKULIA HATUA MKANDARASI WA AWAMU YA PILI MKOA WA PWANI"
Post a Comment