Loading...
title : Wizara ya Afya yazuiya likizo kwa madaktari na wauguzi .
link : Wizara ya Afya yazuiya likizo kwa madaktari na wauguzi .
Wizara ya Afya yazuiya likizo kwa madaktari na wauguzi .
Na Heri Shaaban
NAIBU WAZIRI wa Afya na Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto DKT.Faustine Ndugulile ameziagiza Halmashauri kuangalia upya utoaji wa likizo kwa madaktari na wauguzi katika kipindi cha kufunga mwaka kutokana na idadi ya wagonjwa kuwa kubwa .
Dkt .Ndungulile alisema hayo Wilayani Ilala katika vituo vya afya alivyotembelea jimboni Segerea ambavyo ni Buguruni Plani ,Tabata A na segerea Ugombolwa .
" Kipindi cha mwisho wa mwaka kina changamoto kwa upande wa wagonjwa wanakuwa wengi hivyo kabla kuwapa rikizo taratibu za utoaji zifuatwe lengo wagonjwa waweze kupata huduma kwa wakati" alisema Ndungulile.
Alisema katika ziara yake ameweza kujionea idadi ya wagonjwa wengi wakisubiri matibabu katika vituo vya afya alivyotembelea katika ziara yake hiyo ya kikazi..
Aidha katika hatua nyingine Naibu Waziri Ndungulile amepiga marufuku dawa wagonjwa kuandikiwa kununua nje ya vituo vya afya vya serikali badala yake wagonjwa wote dawa wapewe katika vituo hivyo serikali imenunua dawa za kutosha.
Aliwakikishia wananchi Wizara imeshasambaza dawa katika vituo vya afya nchi nzima lengo kuwapa huduma bora wananchi.
Wakati huohuo ametoa muda wa miezi mitatu Manispaa ya Ilala kuboresha mfumo wa Mapato na Mahabara katika hospitali ya Plani iliyopo Buguruni Mnyamani.
Kwa upande wake Mbunge wa Segerea (CCM)Bonah Kaluwa amemuomba Naibu Waziri kuongea na Serikaki Kuu ili kuarakisha Wakala wa Barabara TARURA kujenga Barabara ya Mnyamani ili wagonjwa wafike kwa wakati kupatiwa matibabu.
"Kilio changu barabara ya Mnyamani wananchi Wangu wanapata shida njia mbovu muda mrefu mpaka sasa hakuna hatua zilizochukuliwa gari la wagonjwa pia linapita kwa shida kupeleka wagonjwa wa rufaa "alisema Kaluwa.
Pia aliomba Wizara kuipandisha adhi zahanati hiyo ya Plani .
Naye Dkt. wa Zamu Msimamizi wa Vitendo Neema Ntabaye alisema madktari waliopo 12 changamoto jengo la upasuaji.
Hivyo makala Wizara ya Afya yazuiya likizo kwa madaktari na wauguzi .
yaani makala yote Wizara ya Afya yazuiya likizo kwa madaktari na wauguzi . Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Wizara ya Afya yazuiya likizo kwa madaktari na wauguzi . mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/12/wizara-ya-afya-yazuiya-likizo-kwa.html
0 Response to "Wizara ya Afya yazuiya likizo kwa madaktari na wauguzi ."
Post a Comment