Loading...
title : NAISINYAI YANYAKUA UBINGWA WA TAKUKURU SIMANJIRO
link : NAISINYAI YANYAKUA UBINGWA WA TAKUKURU SIMANJIRO
NAISINYAI YANYAKUA UBINGWA WA TAKUKURU SIMANJIRO
Na Woinde Shizza,Simanjiro.
Timu ya jamii ya wafugaji wa Naisinyai S. C ya Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, imeshinda ngao ya maadili iliyoandaliwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kwa kuifunga Mirerani SC kwa penalti 6-5.
Katika mchezo huo wa fainali uliochezwa juzi kwenye uwanja wa barafu mji mdogo wa Mirerani, mgeni rasmi alikuwa Katibu Tawala wa Wilaya hiyo Zuwena Omary. Hadi dakika 90 ya mchezo ulipomalizika timu hizo zilikuwa hazijafungana na walipopigiana penalti tano kwa tano hakukuwa na mshindi ndipo wakapigiana penalti moja kwa moja na Naisinyai ikashinda.
Akizungumza wakati wa kukabidhi ngao hiyo ya maadili kwa timu ya Naisinyai,Katibu Tawala Omary alisema jamii inapaswa kupiga vita matumizi ya vitendo vya rushwa kwa kila sehemu. Alisema jamii inapaswa kuzingatia hilo kupitia kauli mbiu ya wajibika, piga vita rushwa, zingatia maadili, haki za binadamu na utawala bora kuelekea uchumi wa kati.
"Tupige vita rushwa kila mahali, kuanzia michezo ni, makazini, polisi, hospitalini, mahakamani na kila eneo ukiona rushwa inatumika toeni taarifa," alisema Omary. Mkuu wa Takukuru wilaya ya Simanjiro Mashauri Elisante alisema mashindano hayo yalishirikisha timu nne za Naisinyai SC, Mirerani SC, Veterani Mirerani za Simanjiro na Tanzanite FC ya wilaya ya Arumeru mkoani Arusha.
Alisema lengo la mashindano hayo ni maadhimisho ya siku ya maadili na haki za binadamu kitaifa na kupiga vita vitendo vya rushwa. Mwenyekiti wa Kijiji cha Naisinyai, Taiko Laizer alisema hii ni mara ya pili kwa mwaka huu timu hiyo kubeba ubingwa wa soka kwani awali walishinda kombe la mbunge wa jimbo la Simanjiro James Ole Millya.
Laizer alisema siri ya ushindi mara mbili kwa mwaka mmoja kwenye timu hiyo ni kuzingatia mazoezi, nidhamu na ushirikiano wa uongozi na wananchi kwa ujumla.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Naisinyai Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, Taiko Laizer akimbeba golikipa wa Naisinyai SC Joseph John baada ya kunyakua ngao ya Takukuru kwa kuifunga Mirerani SC kwa penalti 6-5
Mwenyekiti wa Kijiji cha Naisinyai Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, Taiko Laizer akimbeba golikipa wa Naisinyai SC Joseph John baada ya kunyakua ngao ya Takukuru kwa kuifunga Mirerani SC kwa penalti 6-5
Hivyo makala NAISINYAI YANYAKUA UBINGWA WA TAKUKURU SIMANJIRO
yaani makala yote NAISINYAI YANYAKUA UBINGWA WA TAKUKURU SIMANJIRO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala NAISINYAI YANYAKUA UBINGWA WA TAKUKURU SIMANJIRO mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/12/naisinyai-yanyakua-ubingwa-wa-takukuru.html
0 Response to "NAISINYAI YANYAKUA UBINGWA WA TAKUKURU SIMANJIRO"
Post a Comment