Loading...

Shule ya Macedonia yapanda Kitaaluma

Loading...
Shule ya Macedonia yapanda Kitaaluma - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Shule ya Macedonia yapanda Kitaaluma, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Shule ya Macedonia yapanda Kitaaluma
link : Shule ya Macedonia yapanda Kitaaluma

soma pia


Shule ya Macedonia yapanda Kitaaluma

  



Mwanamuziki Saida Kaloli akitoa Burudani leo katika Shule ya  Msingi Masedonia iliyopo Bonyokwa Wilayani Ilala Dar es Salaam wakati wa Mahafali ya Shule hiyo na siku ya Wazazi.Desemba 25 mwaka huu Saida Kaloli atakuwa akitoa burudani Segerea.Picha na Heri Shaaban

Na. Heri Shaaban 
Mwambawahabari
SHULE ya msingi Macedonia yafanya vizuri kitaaluma mwaka hadi mwaka kwa kushika Alana za juu  ngazi ya Wilaya na Mkoa

Akizungumza Dar es Salaam mwishoni mwa wiki wakati wa kufunga mwaka wa masomo na kuwapongeza wanafunzi waliofanya vizuri Mwalimu Mkuu  wa Macedonia ,Makwasa Masasa, alisema    ilianzishwa January 2009  mahafali ya kwanza ya darasa la saba yalifanyika mwaka 2012 wanafunzi waliopo shule hiyo 843 waliomaliza mwaka  huu 91 wavulana 39 wasichana 52  katika kuhakikisha wanakuza vipaji vya watoto  wamezingatia kuweka masomo ya ziada yakiwemo kompyuta, kifaransa ,Sanaa na scout kwa madarasa yote.

"Shule yetu kitaaluma  ipo vizuri  matokeo ya mitihani ndani na nje   shule inafanya vizuri katika alama za daraja A naB   Mwaka 2016 walikuwa watahiniwa 53 wa darasa la saba wote walifaulu  Vizuri kwa asilimia 100 walipata wastani wa alama 215 . 89 daraja A ambapo wanafunzi walikwenda shule za serikali na Vipaji maalum Masasa.

Masada alisema  wanafunzi wake 47 walipata alama A sita alama B shule ilishika nafasi ya pili kiwilaya kati ya shule 45 na kwa upande wa mkoa ilishika nafasi ya saba kati ya shule 404 ambapo Kitaifa ilishika nafasi ya 18 kati ya shule 8109 ambazo ni kundi la shule  zenye watainiwa zaidi ya 40.

Aidha akielezea zaidi taaluma katika shule hiyo mwaka 2017 wanafunzi wa darasa la saba walikuwa 74  ambapo walifanya vizuri kwa asilimia 100     ufaulu  ambapo shule ilishika nafasi ya kwanza Kiwilaya  Kati ya shule 51  kimkoa nafasi ya tisa kati ya shule 453 na kitaifa nafasi ya 51 kati ya shule 9736.

Alisema anawapongeza Wazazi kwa ushirikiano wa Walimu na watumishi  wameweza kuifikisha shule hiyo na kuwa na wanafunzi wenye maadili mazuri.

"Ushindani ni mkubwa    lakini wamejipanga kuhimili ushindani tunao walimu bora
34      wenye sifa katika taaluma mbali mbali  na shule yetu ni moja ya shule bora" alisema.

Aliwataka Wazazi kuwalea watoto wao katika misingi inayofaa na kuwaimiza kila wakati wazingatie masomo watoto wao ili kuandalia mazingira bora ikiwemo kuwapatia mahitaji yao kitaaluma na kulipa ada kwa wakati.

Akielezea changamoto za shule hiyo   masharti magumu ya mikopo Benki na riba kubwa   Kwa mikopo inayotolewa mashuleni   wakati shule zinatoa huduma kijamii hazijiendeshi kibiashara  ila masharti makubwa  hali inayopelekea kushindwa kufanya upanuzi wa miundombinu ya shule hiyo.

Changamoto nyingine katika shule ya Macedonia ni tatizo la maji safi na salama  ambapo eneo hilo la Bonyokwa Wilayani Ilala limesahaulika kwa kupatiwa miundombinu ya Huduma za maji  hali inayopelekea kununua maji ya kuendeshea shughuli shuleni hapo.

Aliomba Serikali  inapotokea fursa  kwa wanafunzi wa kitanzania  wapewe haki na huduma sawa bila kubagua  shule za watu binafsi na shule za serikali bali haki itendeke.

Kwa upande wake Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Uratibu wa Program ya sekta ya Maji Wizara ya Maji na Umwagiliaji Mhandisi Dorisia Mulashani,alipongeza shule ya Macedonia kwa juhudi na kufanikiwa kitaaluma  ambapo aliwataka Wazazi washirikiane na Walimu wa shule   hiyohiyo katika kukuza taaluma.

Mhandisi Dorisia alisema  shule hiyo  IPO juu kitaaluma ina vipaji mbali mbali   hivyo aliwataka Wazazi kuwalea katika maadili mema  baadae wawewe kuwapata wabunge, Mawaziri , Madaktari  kutokana na wanavyofundishwa katika chumba cha mahabara ya kisasa kwa vitendo.

" Shule yenu ipo vizuri inavutia changamoto ya maji katika shule   nimeipokea nitaibeba na kuifikisha DAWASCO Tabata nikiwa kama Mkurugenzi wa uratibu wa Programu ya sekta ya maji kutoka Wizarani mpaka ifikapo mwakani shule itakuwa na maji na kwa zile kaya ambazo hawana maji waandike barua ya utamburisho kutoka Serikali ya mtaa wako ili uweze kuletewa huduma ya maji" alisema
Dorisia.


Hivyo makala Shule ya Macedonia yapanda Kitaaluma

yaani makala yote Shule ya Macedonia yapanda Kitaaluma Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Shule ya Macedonia yapanda Kitaaluma mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/12/shule-ya-macedonia-yapanda-kitaaluma.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Shule ya Macedonia yapanda Kitaaluma"

Post a Comment

Loading...