Loading...
title : TAARIFA KWA UMMA: UFAFANUZI KUHUSU OFISI ZA TBS ZINAZOHUSIKA NA UTOAJI MIZIGO BANDARINI
link : TAARIFA KWA UMMA: UFAFANUZI KUHUSU OFISI ZA TBS ZINAZOHUSIKA NA UTOAJI MIZIGO BANDARINI
TAARIFA KWA UMMA: UFAFANUZI KUHUSU OFISI ZA TBS ZINAZOHUSIKA NA UTOAJI MIZIGO BANDARINI
2017-12-05
SHIRIKA LA VIWANGO TANZANIA (TBS)
Shirika la Viwango Tanzania (TBS) linapenda kutoa ufafanuzi kuhusu taarifa zilizotolewa kupitia mtandao wa kijamii (Jamii Forum) kuwa Shirika linadidimiza jitihada za Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli zinazotaka Mamlaka zinazohusika na utoaji mizigo bandarini kufanya kazi masaa 24.
Shirika limetii agizo la Mhe. Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli la kufanya kazi masaa 24 bandarini na bandari kavu ambako huduma za kutoa mizigo zinafanyika muda wote, hivyo maafisa wa TBS wanakuwepo muda wote na wateja wanahudumiwa kikamilifu. Pia namba za simu za maafisa wa TBS zimewekwa ubaoni ili kurahisisha utendaji wakati wote.
Pia kwa upande wa bidhaa za mafuta zinazotokana na petroli, sampuli huchukuliwa bandarini mara tu meli inapotia nanga na kupimwa muda huohuo na majibu yanapotoka hurusiwa kushushwa au kurudishwa zilikotoka endapo zitakuwa zimefeli.
Hata hivyo ofisi zingine za TBS zinazohusika na utoaji mizigo bandarini zilizopo jengo la Diplomat, mtaa wa Mkwepu / Kaluta, Karibu na jengo la TTCL Makao Makuu, jijini Dar es Salaam, zinafanya kazi kuanzia saa 1.30 asubuhi mpaka saa 4.00 usiku, hii ni kuanzia siku za Jumatatu mpaka Ijumaa. Siku za jumamosi ofisi hufunguliwa saa 3.00 asubuhi mpaka saa 10.00 jioni. Endapo mteja atahitaji huduma baada ya muda tajwa, Shirika limeweka namba za simu ili kuwawezesha wateja kuendelea kupata huduma endapo kuna uhitaji.
Shirika linaomba radhi kwa wateja kutokana usumbufu uliojitokeza siku Jumamosi ya tarehe 2 Desemba, 2017, kwani ofisi za jengo la Diplomat zilifunguliwa saa 4.00 asubuhi badala ya saa 3.00 asubuhi. Hata hivyo wateja waliofika kuanzia muda huo walihudumiwa kikamilifu na kuendelea na taratibu zingine za kutoa mizigo bandarini.
Shirika linaendelea na jitihada za kuboresha huduma zaidi kwa wateja, ikiwa ni pamoja na kuingia mkataba na benki ya NMB ili wateja waweze kupatiwa huduma za kibenki bandarini hadi usiku. Pia kuanzia sasa ofisi ya TBS katika jengo la Diplomat zitaanza kutoa huduma kuanzia saa 1.30 hadi saa 12.00 jioni kwa siku za Jumamosi
Shirika litaendelea kuunga mkono jitihada za Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwa kuhakikisha kwamba bandari zetu zinatoa huduma bora na zenye tija kwa taifa letu.
Kwa maelezo zaidi wasilianaj na:
Mkurugenzi mkuu
Shirika la Viwango Tanzania (TBS)
S.L.P. 9524, Dar es Salaam
Simu: +255 22 2450298/2450206/2451763-6
Nukushi: +255 22 2450959
Hotline:0800 110 827
Hivyo makala TAARIFA KWA UMMA: UFAFANUZI KUHUSU OFISI ZA TBS ZINAZOHUSIKA NA UTOAJI MIZIGO BANDARINI
yaani makala yote TAARIFA KWA UMMA: UFAFANUZI KUHUSU OFISI ZA TBS ZINAZOHUSIKA NA UTOAJI MIZIGO BANDARINI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TAARIFA KWA UMMA: UFAFANUZI KUHUSU OFISI ZA TBS ZINAZOHUSIKA NA UTOAJI MIZIGO BANDARINI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/12/taarifa-kwa-umma-ufafanuzi-kuhusu-ofisi.html
0 Response to "TAARIFA KWA UMMA: UFAFANUZI KUHUSU OFISI ZA TBS ZINAZOHUSIKA NA UTOAJI MIZIGO BANDARINI"
Post a Comment