Loading...

TUNDU LISSU: NIMEFURAHI SANA MZEE MWINYI KUJA KUNIPA POLE.

Loading...
TUNDU LISSU: NIMEFURAHI SANA MZEE MWINYI KUJA KUNIPA POLE. - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa TUNDU LISSU: NIMEFURAHI SANA MZEE MWINYI KUJA KUNIPA POLE., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : TUNDU LISSU: NIMEFURAHI SANA MZEE MWINYI KUJA KUNIPA POLE.
link : TUNDU LISSU: NIMEFURAHI SANA MZEE MWINYI KUJA KUNIPA POLE.

soma pia


TUNDU LISSU: NIMEFURAHI SANA MZEE MWINYI KUJA KUNIPA POLE.

Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu amesema licha ya umri wa miaka 93 alionao Rais mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi bado amediriki kufunga safari kwenda kumtembelea na kumpa pole.

Lissu, ambaye ni Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), alitoa kauli hiyo muda mfupi baada ya kutembelewa na Mzee Mwinyi katika Hospitali ya Nairobi nchini Kenya ambako anaendelea na matibabu.

Lissu amelazwa hospitalini hapo tangu Septemba 7 anakotibiwa akiuguza majeraha ya kushambuliwa kwa risasi zaidi ya 30 akiwa nyumbani kwake mjini Dodoma akitokea kuhudhuria mkutano wa Bunge.

Akizungumza na Mwananchi jana kwa simu kuhusu kutembelewa na Mzee Mwinyi, mwanasheria huyo wa Chadema pamoja na mke wake, Alice walisema wamefurahi kutembelewa na kiongozi huyo.

“Nimefurahi sana kwamba umri wote alionao wa miaka 93 si kidogo, ametafuta muda kuja kunipa pole hospitalini ni kitu kizuri sana, ni ubinadamu mkubwa sana,” alisema Lissu ambaye alionekana mwenye furaha.

Rais mstaafu Mwinyi anakuwa miongoni mwa viongozi wa juu wa Serikali waliomtembelea Lissu kwani hivi karibuni Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan naye alifika hospitalini hapo kumjulia hali.

Mzee Mwinyi akiambatana na mke wake na maofisa wa ubalozi wa Tanzania nchini Kenya walifika hospitalini hapo kumjulia hali mbunge huyo na picha zinawaonyesha wawili hao wakizungumza huku nyuso zao zikiwa na tabasamu.


Hivyo makala TUNDU LISSU: NIMEFURAHI SANA MZEE MWINYI KUJA KUNIPA POLE.

yaani makala yote TUNDU LISSU: NIMEFURAHI SANA MZEE MWINYI KUJA KUNIPA POLE. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala TUNDU LISSU: NIMEFURAHI SANA MZEE MWINYI KUJA KUNIPA POLE. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/12/tundu-lissu-nimefurahi-sana-mzee-mwinyi.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "TUNDU LISSU: NIMEFURAHI SANA MZEE MWINYI KUJA KUNIPA POLE."

Post a Comment

Loading...