Loading...
title : Upasuaji wa Kihistoria, Aliyepandikizwa Figo Muhimbili Aruhusiwa
link : Upasuaji wa Kihistoria, Aliyepandikizwa Figo Muhimbili Aruhusiwa
Upasuaji wa Kihistoria, Aliyepandikizwa Figo Muhimbili Aruhusiwa
Dar es salaam, Tanzania. Mgonjwa aliyefanyiwa upasuaji wa kihistoria wa kupandikizwa figo leo ameruhusiwa kutoka katika hospitalini akiwa na afya njema.
Bibi Prisca Mwingira ambaye amefanyiwa upasuaji mkubwa na wa kwanza kufanyika hapa nchini alipandikizwa figo Novemba 21, mwaka huu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) chini ya timu ya wataalam wa MNH kwa kushirikiana na watalaam wa Hospitali ya BLK ya nchini India.
Akizungumza na waandishi wa habari leo baada ya kuruhusiwa kutoka hospitalini Bibi Prisca amewashukuru watalaamu wote walioshiriki katika kumuhudumia na pia ametumia fursa huyo kumuomba Rais John Magufulu kuendelea kuisaidia MNH ili kuhakikisha huduma za kibingwa wa juu zinaendelea kutolewa katika hospitali hiyo.
“Kipekee namshukuru mwenyezi Mungu, madaktari , wauguzi, uongozi wa Hospitali ya Muhimbili pamoja na serikali kwa kufanisha matibabu yangu, nilisumbuliwa na ugonjwa wa figo takribani mwaka mzima na kuingia katika matibabu ya kuchuja damu, lakini hatimaye leo kaka yangu amejitolea figo yake moja na nimewekewa mimi kwa kweli namshukuru sana.
“Napenda kuwashauri wagonjwa wenye matatizo ya figo na wanaoendelea na huduma ya kuchuja damu wasikake tamaa kwani sasa matibabu yamepatikana na mimi ni shuhuda katika hili,’’ amesema Bibi Prisca.
Bibi Prisca Mwingira ambaye alifanyiwa upasuaji wa kupandikizwa figo Novemba 21, mwaka huu akiishukuru Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), madaktari bingwa wa hospitali hiyo pamoja na Rais John Pombe Magufuli baada ya afya yake kuendelea vizuri. Bibi Prisca ameruhusiwa kurejea nyumbani leo saa 6:00 mchana baada madaktari bingwa wa magonjwa figo kufanikisha upasuaji huo wa kihistoria. Kulia ni Bathelomayo Mwingira ambaye amempatia dada yake figo. Kushoto ni Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Figo, Dkt. Jacqueline Shoo, Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Figo Dkt. Kisanga (katikati), wote wa Muhimbili.
Bibi Prisca Mwingira akimshukuru kaka yake, Bathelomayo Mwingira kwa kumpatia figo kutokana na tatizo hilo kumsumbua katika kipindi cha mwaka mmoja.
Baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali nchini wakishudia tukio hilo lakihistoria ambalo limefanywa na madaktari bingwa wa Muhimbili.
Hivyo makala Upasuaji wa Kihistoria, Aliyepandikizwa Figo Muhimbili Aruhusiwa
yaani makala yote Upasuaji wa Kihistoria, Aliyepandikizwa Figo Muhimbili Aruhusiwa Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Upasuaji wa Kihistoria, Aliyepandikizwa Figo Muhimbili Aruhusiwa mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/12/upasuaji-wa-kihistoria-aliyepandikizwa.html
0 Response to "Upasuaji wa Kihistoria, Aliyepandikizwa Figo Muhimbili Aruhusiwa"
Post a Comment