Loading...
title : VIONGOZI WA UMMA WATAKIWA KUKABIDHI ORODHA YA MALI ZAO KABLA YA DESEMBA 31
link : VIONGOZI WA UMMA WATAKIWA KUKABIDHI ORODHA YA MALI ZAO KABLA YA DESEMBA 31
VIONGOZI WA UMMA WATAKIWA KUKABIDHI ORODHA YA MALI ZAO KABLA YA DESEMBA 31
VIONGOZI
wote wa umma nchini wametakiwa kuorodhesha mali zao tena kwa usahihi na
kisha kukabidhi kwa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kabla
ya Desemba 31 mwaka huu.
Wamesisitiza kufanya hivyo ni utaratibu
ambao upo kwa mujibu wa sheria ,hivyo lazima watekeleze kwa wakati na
watakaoshindwa hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.
Hayo
yamesemwa Dar es Salaam leo na Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya
Viongozi wa Umma, Jaji Mstaafu Harold Nsekela wakati akitangza tarehe ya
mwisho kwa viongozi wa umma kukabidhi tamko la mali zao ambayo ni
Desemba 31 mwaka huu.
“Kila kiongozi wa umma ajaze tamko hilo
kwa kuorodhesha mali zake, mwenza wake na watoto wake walio na umri
chini ya miaka 18,”amesema. Amefafanua viongozi wanaotakiwa kuorodhesha
mali zao na kisha kukabidhi Sekretarieti ya Maadili ni wale wa
kuteuliwa na kuchaguliwa.
“Pia ujazaji wa tamko hilo kisheria
linawahusisha hata viongozi waliostaafu na wale wanaoelekea
kustaafu,”amesisitiza. Ameongeza viongozi ambao wanastaafu wakati
wanaingia waliorodhesha mali zao, hivyo wanapostaafu ni lazima
waoredheshe ili ifahamike wanatoka wakiwa na mali kiasi gani.
“Hivyo
ni muhimu kila kiongozi kujaza hilo tamko na tunachokifanya sisi ni
kukumbusha tu.Fomu za tamko zipo kwenye tovuti ya sekretarieti ya
maadili. “Huko nyuma tulikuwa tunawatafuta viongozi na kuwapa matamko
wajaze lakini sasa ni lazima wao kuchukua na kujaza na jukumu letu ni
kupokea na kisha kuchambua tamko la kila kiongozi,”amesema Jaji mstaafu
Nsekela.
Amesema anaamini viongozi wanafahamu wajibu wao,hivyo
wafanye haraka iwezekanavyo na hasa kwa kuzingatia muda uliobakia ni
mchache. Alipoulizwa ni viongozi wangapi wamejaza fomu hadi sasa,Jaji
mstaafu Nsekela amesema hana takwimu sahihi lakini baada ya muda
ulioapngwa kumaliza watatoa taarifa sahihi huku akieleza yeye tayari
ameorodhesha mali zake kwenye tamko na kukabidhi tena kwa Rais.
Kuhusu
viongozi wanaostaafu ambao wamejaza tamko hilo amesema nao bado lakini
katika eneo hilo kuna changamoto yake kidogo kwani viongozi wanapostaafu
inakuwa ngumu kuwapata lakini nao watambue wanatakiwa kujaza tamko kwa
mujibu wa sheria.
Kwa upande wake, Ofisa Sheria Mkuu wa
Sekretarieti ya Mmaadili Bw. Filotheus Manula ameongeza ujazaji wa
tamko la mali kwa viongozi wa umma ni takwa la kikatiba na kuna adhabu
kwa wasiofuata.
Ametaja adhabu hizo ni kuonywa, kushushwa cheo, kusimamishwa kazi na wakati mwingine kufukuzwa Nazi.
Na Said Mwishehe,Blogu ya Jamii
.
Hivyo makala VIONGOZI WA UMMA WATAKIWA KUKABIDHI ORODHA YA MALI ZAO KABLA YA DESEMBA 31
yaani makala yote VIONGOZI WA UMMA WATAKIWA KUKABIDHI ORODHA YA MALI ZAO KABLA YA DESEMBA 31 Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala VIONGOZI WA UMMA WATAKIWA KUKABIDHI ORODHA YA MALI ZAO KABLA YA DESEMBA 31 mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/12/viongozi-wa-umma-watakiwa-kukabidhi_27.html
0 Response to "VIONGOZI WA UMMA WATAKIWA KUKABIDHI ORODHA YA MALI ZAO KABLA YA DESEMBA 31"
Post a Comment