Loading...
title : WACHIMBAJI WA JASI WALILIA SOKO LA UHAKIKA
link : WACHIMBAJI WA JASI WALILIA SOKO LA UHAKIKA
WACHIMBAJI WA JASI WALILIA SOKO LA UHAKIKA
Wachimbaji wa Madini ya Jasi Mkoani Singida wametakiwa kufanya shughuli zao kwa uaminifu ili kujihakikishia soko la uhakika.
Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo ametoa wito huo Desemba 11, 2017 Wilayani Itigi mara baada ya kuzungumza na Wachimbaji wa madini hayo wakati wa ziara yake kwenye maeneo yenye uchimbaji wa madini ya Jasi Mkoani Singida.
Wachimbaji wa Madini hayo walimueleza Naibu Waziri Nyongo changamoto mbalimbali zinazowakabili ikiwemo ukosefu wa soko la uhakika.
Mara baada ya wachimbaji hao kuelezea changamoto zinazowakabili, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Itigi, Ali Minja alimueleza Naibu Waziri Nyongo kwamba tatizo la soko la Madini ya Jasi yanayochimbwa Singida linasababishwa na wachimbaji wenyewe kwa kuchanganya madini hayo na udongo.
Alisema wakati mwingine wachimbaji wenyewe wanasababisha kupotea kwa soko, kwani mnunuzi akinunua Madini ya Jasi yaliyochanganywa na udongo hawezi kurudi tena kununua.“Baadhi ya wachimbaji wa Jasi Mkoani hapa sio waaminifu kwani wanachanganya madini na takataka ikiwemo udongo, na hii inakimbiza wanunuzi,” alisema.
Kufuatia hali hiyo, Naibu Waziri Nyongo aliwaasa wachimbaji hao kuwa wakweli kwa kufanya shughuli zao kwa uadilifu na ubunifu mkubwa wa utafutaji wa masoko ili kuvutia wanunuzi wengi zaidi na hivyo kujiongezea kipato.
Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Kati Singida, Sosthenes Massola (kushoto) akizungumza na Wafanyakazi, Wachimbaji na Wafanyabiashara wa Madini ya Jasi (hawapo pichani) wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (kulia aliyesimama) Mkoani Singida.
Mkurugenzi wa Kiwanda cha Kutengeneza Mapambo ya majumbani cha RSR kilichopo Singida Mjini, Rashid Rashid (kushoto) akimuonesha Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (kulia) baadhi ya bidhaa zinazozalishwa kiwandani hapo zitokanazo na Madini ya Jasi yanayochimbwa Itigi mkoani humo.
Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (aliyesimama) akizungumza na Wafanyakazi, Wachimbaji na Wafanyabiashara wa Madini ya Jasi (hawapo pichani) wakati wa ziara yake Itigi Mkoani Singida. Kushoto ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Itigi, Pius Luhende.
Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (katikati) akitembelea Kiwanda cha kutengeneza Chaki cha Furaha, kilichopo katika Kata ya Tambukareli, Itigi. Kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Itigi, Pius Luhende na kushoto ni Meneja wa Kiwanda hicho, Peter Nolasco.
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala WACHIMBAJI WA JASI WALILIA SOKO LA UHAKIKA
yaani makala yote WACHIMBAJI WA JASI WALILIA SOKO LA UHAKIKA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WACHIMBAJI WA JASI WALILIA SOKO LA UHAKIKA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/12/wachimbaji-wa-jasi-walilia-soko-la.html
0 Response to "WACHIMBAJI WA JASI WALILIA SOKO LA UHAKIKA"
Post a Comment