Loading...
title : Watanzania wanaoishi Saudi Arabia wakutana kwa majadiliano
link : Watanzania wanaoishi Saudi Arabia wakutana kwa majadiliano
Watanzania wanaoishi Saudi Arabia wakutana kwa majadiliano
Na Mwandishi Maalum, Saudi Arabia
Jumuiya ya Watanzania waishio Jeddah nchini Saudi Arabia ' Tanzania Welfare Society' hivi karibuni ilifanya Mkutano wa pamoja wa wanajumuiya Watanzania na Wanadiaspora. Mkutano huo pia ulihudhuriwa na Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia Mhe. Hemedi Mgaza. Aidha, mkutano huo ulihudhuriwa na Spika Mstaafu wa Balaza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Pandu Amir Kificho ambaye alikuwa mgeni rasmi. Mhe. Pandu Amir Kificho alikuwa nchini Saudi Arabia kutekeleza ibada ya 'Umrah' katika miji ya Makkah na Madina.
Wanajumuiya walipata fursa ya kusikiliza hotuba zilizotolewa na Balozi na Spika Mstaafu wa Balaza la Wawakilishi. Vile vile waliweza kuuliza maswali na pia kutoa maoni na ushauri.
Katika hotuba zilizotolewa wanajumuiya walisisitizwa kuwa na umoja na uzalendo kwa Tanzania. Walitakiwa kufanya kazi kwa bidii na kuhakikisha wanachangia maendeleo ya Tanzania. Habari zimeletwa na Mwandishi Maalumu wa Jeddah, Saudi Arabia. Kwa Picha na matukio mengine zaidi angalia youtube kupitia 'Prince eddycool'
Kutoka Kushoto Afisa Utawala wa Konseli Kuu ya Jeddah Ali Mohamed, Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia Mhe. Hemedi Mgaza, Spika Mstaafu wa Baraza la Wawakilishi Zanziabar Mhe. Pandu Amir Kificho ambaye alikuwa mgeni mwalikwa, Kaimu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania waishio mji wa Jeddah Bw. Salim Ali Shatri.
Baadhi ya Watanzania na wanadiaspora wa Jeddah wakiwa katika picha na meza kuu baada ya mkutano.
Watanzania na Wanadiaspora wa Jeddah wakisikiliza hotuba katika hoteli ya Trident.
Hivyo makala Watanzania wanaoishi Saudi Arabia wakutana kwa majadiliano
yaani makala yote Watanzania wanaoishi Saudi Arabia wakutana kwa majadiliano Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Watanzania wanaoishi Saudi Arabia wakutana kwa majadiliano mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/12/watanzania-wanaoishi-saudi-arabia.html
0 Response to "Watanzania wanaoishi Saudi Arabia wakutana kwa majadiliano"
Post a Comment