Loading...
title : WATANZANIA WAOMBA KUSHIRIKI MKESHA MKUBWA KITAIFA,DUA MAALUMU
link : WATANZANIA WAOMBA KUSHIRIKI MKESHA MKUBWA KITAIFA,DUA MAALUMU
WATANZANIA WAOMBA KUSHIRIKI MKESHA MKUBWA KITAIFA,DUA MAALUMU
Said Mwishehe, Blogu ya jamii
WANZANIA wameombwa kushiriki katika mkesha mkubwa kitaifa ambao pia utatumika kufanya maombi maalumu kumuombea Rais John Magufuli.
Mkesha huo unatarajia kufanyika Desemba 31 mwaka huu katika Uwanja wa Uhuru uliopo jijini Dar es Salaam.
Akizungumza Dar es Salaam leo, Askofu Dk. Godfrey Malassy kwa niaba ya Tanzania Fellowship of Churches amesema mwaka huu ni mwaka wa pekee kwa Taifa la Tanzania kufuatia matendo makuu ambayo Mungu ameitendea nchini yetu.
“Na hasa ni kutokana na kazi njema inayofanywa na Serikali ya Awamu ya tano chini uongozi wa Rais Magufuli na wasaidizi wake wote kuonesha mwanga na dira katika usimamizi wa rasilimali zote za Taifa.
“Tunamshukuru Mungu kwamba amesikia maombi yetu Watanzania. Leo watanzania na ulimwengu mzima ni mashahidi wa Tanzania mpya yenye amani na utulivu unaotoa fursa kwa wananchi wote kufanya kazi kwa bidii na kujenga uchumi,” amesema Dk.Malassy.
Ameongeza mwaka 2017 ni mwaka wa kipekee kwa Taifa, hivyo ni fursa adhimu kwa Watanzania wote kukusanyika nchini nzima kwa sauti moja kusimama pamoja usiku wa Desemba 31 kumshukuru Mungu kwa kutuvusha mwaka huu.
“Hivyo tuombe kwa ajili ya kuukaribisha mwaka 2018. Mwaka huu tunasababu muhimu kitaifa kumuombea Rais Magufuli kwa jukumu kubwa alilokabidhiwa na kila Mtanzania kuongoza Taifa letu la Tanzania,”amesema.
Amefafanua maono ya mkesha mkubwa kitaifa utakaombatana na maombi maalum kwa Taifa umelenga Taifa liwe na amani na utulivu toka kwa Mungu wa amani aliye hai.
“Hakuna amani bila Mungu yeye ndiye mtoa amani kwa watu wote wamchao kwa kusudi lake. Mungu analokusudia na Taifa hili,”amesema.
Amesema amani ni msingi wa maisha ya mwanadamu na bila amani maisha yanakuwa magumu.
Ametaja mikoa mingine ambayo mkesha huo utafanyika Desemba 31 mwaka huu ni Dodoma, Kilimanjaro, Mwanza, Iringa, Ruvuma, Singida, Morogoro na Zanzibar
Viongozi wa kamati ya maandalizi wakiongozwa na Askofu, Dk.Godfrey Malasy(wa tatu kulia) wakizungumza leo jijini Dar es Salaam kuhusu mkesha mkubwa kitaifa unaotarajia kufanyika Desemba 31 mwaka huu katika mikoa 10 nchini.
Hivyo makala WATANZANIA WAOMBA KUSHIRIKI MKESHA MKUBWA KITAIFA,DUA MAALUMU
yaani makala yote WATANZANIA WAOMBA KUSHIRIKI MKESHA MKUBWA KITAIFA,DUA MAALUMU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WATANZANIA WAOMBA KUSHIRIKI MKESHA MKUBWA KITAIFA,DUA MAALUMU mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/12/watanzania-waomba-kushiriki-mkesha.html
0 Response to "WATANZANIA WAOMBA KUSHIRIKI MKESHA MKUBWA KITAIFA,DUA MAALUMU"
Post a Comment