Loading...
title : Zanzibar Heroes yaingia Fainali CECAFA yaifunga Uganda Cranes 2-1
link : Zanzibar Heroes yaingia Fainali CECAFA yaifunga Uganda Cranes 2-1
Zanzibar Heroes yaingia Fainali CECAFA yaifunga Uganda Cranes 2-1
Kungo wa Uganda Allan Kaymbadde akifanya maarifa kumpita beki wa Zanzibar Heroes Abdallah Salum katika mchezo wa Nusu Fainali ya Cecafa. Zanzibar Heroes imeshinda 2-1 na kuingia fainali ambapo itapambana na Harambee Stars ya Kenya
Timu ya Taifa ya Zanzibar , Zanzibar Heroes imefanikiwa kuingia fainali ya CECAFA baada ya kuwaondoa mabingwa watetezi Uganda Cranes katika mchezo wa nusu fainali uliofanyuika Moi Stadium Kisumu, Kenya
Alikuwa ni kiungo Abdul aziz Makame aliyewainua wazanzibari dakiki ya 22 ya mchezo baada ya kuwafunga Waganda waliozemmbea kuokoa kona iliyopigwa .
Hata hivyo Uganda Cranes waliamka na kufanya mashambulizi dhidi ya Zanzibar na kufanikiwa kusawazisha dakika ya 37 ya mchezo kupitia Derrick Nsibambi.
Hadi mapumziko timu hizi zilikuwa sare na hakuna mbabe.
Kipindi cha pili kilianza kwa mashambulizi ya kila pande hata hivyo ilikuwa ni Zanzibar iliyofanikiwa kupata goli la pili lililofungwa kwa njia ya Penelti na kiungo Mohammed Issa "Banka" katika dakika ya 57 ya mchezo .baada ya Joseph Nsubuga kumwangusha Ibrahim Hamad Hilika ndani ya kumi na nane. Joseph pia alilimwa kadi nyekundu
Ugandi ilizidisha mashambulizi lakini ngome ya Zanzibar ilisimama imara hadio mwisho wa mchezo.
Zanzibar Heroes itakutana na wenyeji Kenya Harambee Stars siku ya Jumapili katika mchezo wa fainali. Katika mchezo wa makundu timu hizi zilipokutana zilitoka sare ya kutofungana
Kila la kheri Zanzibar Heroes
Hivyo makala Zanzibar Heroes yaingia Fainali CECAFA yaifunga Uganda Cranes 2-1
yaani makala yote Zanzibar Heroes yaingia Fainali CECAFA yaifunga Uganda Cranes 2-1 Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Zanzibar Heroes yaingia Fainali CECAFA yaifunga Uganda Cranes 2-1 mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/12/zanzibar-heroes-yaingia-fainali-cecafa.html
0 Response to "Zanzibar Heroes yaingia Fainali CECAFA yaifunga Uganda Cranes 2-1"
Post a Comment