Loading...
title : MAVUNDE AWADUWAZA WANAKIJIJI WA MATUMBULU KWA KUKAMILISHA AHADI YAKE.
link : MAVUNDE AWADUWAZA WANAKIJIJI WA MATUMBULU KWA KUKAMILISHA AHADI YAKE.
MAVUNDE AWADUWAZA WANAKIJIJI WA MATUMBULU KWA KUKAMILISHA AHADI YAKE.
Mbunge wa Jimbo la Dodoma Anthony Mavunde ameendelea kutekeleza ahadi zake alizoahidi wakati wa kampeni ya uchaguzi Mkuu wa 2015 ambapo leo amekamilisha ahadi yake ya kutatua kero ya maji katika kijiji cha Matumbulu.
Mavunde amekamilisha ahadi yake ya kutatua kero hiyo kwa kutoa mabomba ya kusambazia maji kijiji kizima yenye urefu wa Kilomita 1 yenye thamani ya zaidi ya Sh.Milioni 8.
Kufuatia utekelezaji huo wa ahadi hiyo, wananchi hao walishikwa na butwaa kwa uharaka wa utekelezaji wa ahadi hiyo kwakuwa tatizo hilo la upatikanaji wa maji katika eneo ilikuwa ya muda mrefu hali iliyosababisha wananchi kutumia maji yasiyo safi na salama.
Wananchi walikuwa wanakosa fursa ya kupata maji kwa urahisi na hivyo kuwalazimu kutembea umbali mrefu kutafuta maji na muda mwingine kutumia maji ambayo si safi na salama kutoka na umbali wa kufuata maji.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kijiji cha Matumbulu Alfred Malogo, amefurahishwa na utekelezaji wa ahadi hiyo na kwamba alichokifanya Mavunde kuwapatia wakazi wa kijiji hicho mabomba kwa ajili ya kusambazia maji kitatatua kero yao ya muda mrefu ya upatikanaji wa maji.
Mbunge wa Dodoma mjini Anthony Mavunde akikabidhi mabomba ya kusambazia maji katika kijiji cha Matumbulu.
Mbunge wa Dodoma mjini Anthony Mavunde akikabidhi mabomba ya kusambazia maji katika kijiji cha Matumbulu kwa wananchi.
.Mabomba ya kusambazia maji katika kijiji cha Matumbulu
Mbunge wa Dodoma mjini Anthony Mavunde akizungumza na Diwani wa Kata ya Matumbulu Emmanuel Chibago.
Hivyo makala MAVUNDE AWADUWAZA WANAKIJIJI WA MATUMBULU KWA KUKAMILISHA AHADI YAKE.
yaani makala yote MAVUNDE AWADUWAZA WANAKIJIJI WA MATUMBULU KWA KUKAMILISHA AHADI YAKE. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MAVUNDE AWADUWAZA WANAKIJIJI WA MATUMBULU KWA KUKAMILISHA AHADI YAKE. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/07/mavunde-awaduwaza-wanakijiji-wa.html
0 Response to "MAVUNDE AWADUWAZA WANAKIJIJI WA MATUMBULU KWA KUKAMILISHA AHADI YAKE."
Post a Comment