Loading...
title : AMISI TAMBWE AREJEA JIJINI DAR KWA MATIBABU
link : AMISI TAMBWE AREJEA JIJINI DAR KWA MATIBABU
AMISI TAMBWE AREJEA JIJINI DAR KWA MATIBABU
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
BAADA ya kushindwa kucheza katika michuano ya kombe la Mapinduzi kutokana na kuwa na Malaria, mshambuliaji wa kimataifa kutoka Burundi Amisi Tambwe amereja Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya matibabu zaidi.
Tambwe amepanda boti mchana huu visiwani Zanzibar kurejea Dar es Salaam kwa ajili ya matibabu.Daktari wa Yanga SC, Edward Bavu amesema Tambwe amelazimika kuondoka kambini mjini Zanzibar kurejea Dar es Salaam kwa ajili ya matibabu zaidi ya Malaria.
“Ana Malaria, kwa siku zaidi ya nne sasa amekuwa na wakati mgumu, tumelazimika kumrejesha Dar es Salaam ili apatiwe matibabu zaidi,” amesema Dk. Bavu.
Tambwe anaondoka wakati Yanga leo inashuka dimbani kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar kuvaana na Singida United katika mchezo wa mwisho wa kundi B utakaoanza Saa 2:15 usiku.
Mrundi huyo amekuwa katika msimu mgumu, akianza kukaa nje tangu Agosti kutokana na maumivu ya goti kabla ya kurejea Desemba, lakini mapema Januari hii tena anaondolewa kambini kwa sababu ya Malaria.
Na hii inazidi kuipunguzia nguvu safu ya ushambuliaji ya Yanga kipindi hiki ambacho inawakosa wakali wake wengine wazoefu, Mzimbabwe Donald Ngoma na Mzambia, Obrey Chirwa.
Yanga sasa itaendelea kumtegemea Ibrahim Ajib, Mateo Antony,Juma Mahadhi na Yohana Mkomola.
Hivyo makala AMISI TAMBWE AREJEA JIJINI DAR KWA MATIBABU
yaani makala yote AMISI TAMBWE AREJEA JIJINI DAR KWA MATIBABU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala AMISI TAMBWE AREJEA JIJINI DAR KWA MATIBABU mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/01/amisi-tambwe-arejea-jijini-dar-kwa.html
0 Response to "AMISI TAMBWE AREJEA JIJINI DAR KWA MATIBABU"
Post a Comment