Loading...
title : Dkt. Kalemani akagua miradi ya uzalishaji Umeme Katavi
link : Dkt. Kalemani akagua miradi ya uzalishaji Umeme Katavi
Dkt. Kalemani akagua miradi ya uzalishaji Umeme Katavi
Na Teresia Mhagama, Katavi
Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani, amefanya ziara mkoani Katavi kwa lengo la kufuatilia utekelezaji wa maagizo aliyoyatoa kwa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), mwaka 2017 ya kukamilisha ufungaji wa mitambo mipya ya kuzalisha umeme katika wilaya ya Mpanda na Mlele mkoani humo.
Dkt. Kalemani alitoa maagizo hayo baada ya mitambo iliyokuwepo katika kituo cha Mpanda kuharibika na hivyo kupelekea mkoa huo kuwa na changamoto ya upatikanaji wa umeme huku baadhi ya maeneo katika wilaya ya Mlele yakipata umeme kutoka nchini Zambia.
Meneja Miradi kutoka TANESCO, Stephen Manda alimweleza Dkt Kalemani kuwa, ufungaji wa mitambo ya umeme katika kituo cha Mpanda umekamilika na sasa kituo kinazalisha umeme wa kiasi cha megawati 2.5 huku matumizi ya wilaya ya Mpanda yakiwa ni megawati 2.3.
Manda alieleza kuwa, kukamilika kwa mitambo ya umeme katika kituo cha Mpanda kumewezesha vijiji 14 kusambaziwa umeme ikiwemo wilaya mpya ya Tanganyika ambayo imepata umeme kwa mara ya kwanza kutoka kuanzishwa kwake.
Akiwa katika wilaya ya Mlele, Dkt. Kalemani alielezwa kuwa, ufungaji wa mashine moja ya kuzalisha umeme yenye uwezo wa kilowati 476 umekamilika na kuwezesha baadhi ya wakazi wa Mlele hususan Makao Makuu ya wilaya hiyo (Inyonga) kupata umeme.
Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani ( wa nne kulia) na Mkuu wa mkoa wa Katavi, Meja Jenerali (Mst), Raphael Muhuga (wa tano kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa Wizara ya Nishati, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Katavi kabla ya kuanza ziara ya kukagua miradi ya kuzalisha umeme mkoani Katavi.
Meneja Miradi kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Makao Makuu, Stephen Manda (kulia), akitoa maelezo kuhusu mitambo ya uzalishaji umeme katika kituo cha Mpanda mkoani Katavi. Anayesikiliza ni Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani ( katikati) na Mkuu wa mkoa wa Katavi, Meja Jenerali (Mst), Raphael Muhuga (wa kwanza kushoto).
Mitambo ya umeme katika kituo cha Mpanda mkoani Katavi inayozalisha umeme wa kiasi cha megawati 2.5 kwa kutumia mafuta.
Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (kulia) akizungumza na wananchi wa Inyonge wilayani Mlele wakati alipofika wilayani humo kukagua mradi wa uzalishaji umeme.
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala Dkt. Kalemani akagua miradi ya uzalishaji Umeme Katavi
yaani makala yote Dkt. Kalemani akagua miradi ya uzalishaji Umeme Katavi Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Dkt. Kalemani akagua miradi ya uzalishaji Umeme Katavi mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/01/dkt-kalemani-akagua-miradi-ya.html
0 Response to "Dkt. Kalemani akagua miradi ya uzalishaji Umeme Katavi"
Post a Comment