Loading...
title : Jafo Apiga Marufuku Madarasa ya Udongo na Tembe.
link : Jafo Apiga Marufuku Madarasa ya Udongo na Tembe.
Jafo Apiga Marufuku Madarasa ya Udongo na Tembe.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo amewaagiza Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halamshauri zote nchini kuhakikisha wanajenga madarasa yenye ubora na Viwango kuondokana na tatizo la baadhi ya Wilaya kuwa na majengo ya udongo na tembe.
Jafo ametoa agizo hilo leo Mjini Dodoma alipokuwa akifungua mafunzo ya uongozi ya siku tano kwa Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi toka mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Tanga, Pwani, Lindi na Mtwara yanayondelea katika ukumbi wa Hazina mkoani humo.
"Sitaki kuona madarasa ya udongo, tembe na watoto kusomea nje, hakikisheni matumizi ya mapato ya ndani yanagusa na kujibu matatizo ya wananchi," alisisitiza Jafo.Jafo amewataka Wakuu wa Wilaya kuhakikisha matumizi ya mapato ya ndani katika Halmashauri zao yanatumika katika miradi mbalimbali ya wananchi ikiwemo ujenzi wa madarasa ili kuondokana na uwepo wa madara ya udongo na tembe katika halmashauri zote hapa nchi.
Aidha amewataka Wakurugenzi wa Halmashauri kufanya maamuzi ya haraka mara wanapopokea fedha za miradi ya maendeleo, kauli hii imetokana na baadhi ya wakurugenzi kuwa na uzembe katika kufanya maamuzi hivyo kuchelewesha utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika wilaya zao na Taifa kwa ujumla.
Hivyo makala Jafo Apiga Marufuku Madarasa ya Udongo na Tembe.
yaani makala yote Jafo Apiga Marufuku Madarasa ya Udongo na Tembe. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Jafo Apiga Marufuku Madarasa ya Udongo na Tembe. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/01/jafo-apiga-marufuku-madarasa-ya-udongo.html
0 Response to "Jafo Apiga Marufuku Madarasa ya Udongo na Tembe."
Post a Comment