Loading...
title : JAJI MKUU AZINDUA KITUO CHA MAFUNZO, HABARI KUWAJENGEA UWEZO WATUMISHI
link : JAJI MKUU AZINDUA KITUO CHA MAFUNZO, HABARI KUWAJENGEA UWEZO WATUMISHI
JAJI MKUU AZINDUA KITUO CHA MAFUNZO, HABARI KUWAJENGEA UWEZO WATUMISHI
Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.
JAJI Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Juma amezindua Kituo cha Mafunzo na Habari za Mahakama kilichopo Kisutu Dar es Salaam ambacho kitasaidia kuwajengea uwezo watumishi wa Mahakama.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo uliofanyika mapema leo jijini Dar es Salaam Jaji mkuu amesema kituo hicho kina malengo kadhaa ikiwemo kuhakikisha haki inawafikia wananchi na walengwa kwa urahisi zaidi.
Amesema katika kituo jicho kuna vielelezo vingi vya mahakama kutekeleza majukumu yake kwa vitendo, kuwajengea uwezo watumishi wa mahakama hasa kujifunza mambo ambayo kwa Bahati mbaya hawakusoma wakiwa chuoni.Amesema Tehama inarahisisha kazi kwa sababu kutoa haki kwa kutumia tehama wanawafikia wananchi wengi kwa urahisi zaidi.
Prof.Juma amesema kituo hicho ambacho kimejengwa kwa kushirikiana na Benki ya Dunia kitakuwa na maeneo mapya kabisa ambayo yanatakiwa kufanyiwa kazi na watumishi wa mahakama ambayo ni Makosa ya Mtandaoa, Makosa yanayotokana na miamala ya simu na Dawa za kulevya
Amesema mahakimu na waendesha mashtaka wakipata mafunzo hayo watakuwa na uelewa mmoja katika kutoa haki." Makosa hayo matatu yanahitaji ushiriki wa vyombo vya nje, kuna sheria nyingi za kimataifa zinagusa sheria zetu za Tanzania" amesema Ptof.Juma.
Amesema kwa sasa wanapata taarifa za Mahakama kutoka katika mahakama ya Hakimu Mkazi kisutu lakini bado hawajaweza kupata taarifa katika mahakama zote nchini na kuwataka watumishi wa mahakama wawasaidie kukusanya taarifa hizo.Kwa upande wa Mkurugenzi Mkazi wa benki ya Dunia, Bella Bird amesema mfumo huo huo mpya utasaidia kuwafikia wananchi wengi kwa urahisi zaidi.
Naye Mkuu wa Chuo cha Lushoto Paul Kihwelu amesema kwa mara ya kwanza Mahakama imejenga kituo cha mafunzo ambacho ni msingi mzuri wa kuwepo kwa uhuru wa mahakama kwa kuwajengea uwezo watumishi.
"Mafunzo ya mwanzo ya tehama yatatolewa pia kwa wadau mbalimbali wakiwemo wanafunzi, Taasisi ya kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru)" amesema.
Hivyo makala JAJI MKUU AZINDUA KITUO CHA MAFUNZO, HABARI KUWAJENGEA UWEZO WATUMISHI
yaani makala yote JAJI MKUU AZINDUA KITUO CHA MAFUNZO, HABARI KUWAJENGEA UWEZO WATUMISHI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala JAJI MKUU AZINDUA KITUO CHA MAFUNZO, HABARI KUWAJENGEA UWEZO WATUMISHI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/01/jaji-mkuu-azindua-kituo-cha-mafunzo.html
0 Response to "JAJI MKUU AZINDUA KITUO CHA MAFUNZO, HABARI KUWAJENGEA UWEZO WATUMISHI"
Post a Comment