Loading...

MBULU YAPITISHA MPANGO WA BAJETI YA MABILIONI KUKAMILISHA VIPAUMBELE VYAKE

Loading...
MBULU YAPITISHA MPANGO WA BAJETI YA MABILIONI KUKAMILISHA VIPAUMBELE VYAKE - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MBULU YAPITISHA MPANGO WA BAJETI YA MABILIONI KUKAMILISHA VIPAUMBELE VYAKE, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MBULU YAPITISHA MPANGO WA BAJETI YA MABILIONI KUKAMILISHA VIPAUMBELE VYAKE
link : MBULU YAPITISHA MPANGO WA BAJETI YA MABILIONI KUKAMILISHA VIPAUMBELE VYAKE

soma pia


MBULU YAPITISHA MPANGO WA BAJETI YA MABILIONI KUKAMILISHA VIPAUMBELE VYAKE

Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Mkoani Manyara, limepitisha shilingi bilioni 43.983 za mapendekezo ya mpango wa bajeti kwa mwaka wa fedha wa 2018/2019. 

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu, Hudson Kamoga akizungumza baada ya kupitishwa bajeti hiyo, alisema vipaumbele vyake ni elimu, afya, maji, kilimo na mifugo. Kamoga alisema bajeti hiyo imezingatia vipaumbele vya vijiji, kata, halmashauri, mkoa, mpango wa pili wa maendeleo ya Taifa na dira ya maendeleo ya Taifa ya mwaka 2025. 

Alisema vipaumbele vingine ni mikakati na sera mbalimbali za kisekta, maelekezo mbalimbali ya viongozi wakuu wa kitaifa, na ahadi ya Rais John Magufuli alizozitoa wakati wa kampeni wilayani Mbulu. Alisema halmashauri hiyo imejikita katika kuongeza mapato ya ndani kwa kuimarisha vyanzo vilivyopo, kubuni vyanzo vipya na kuimarisha mfumo wa kielectroniki. 

"Halmashauri imejikita katika mpango bora wa matumizi ya ardhi kwa makazi, biashara, viwanda vidogo, maeneo ya malisho ya mifugo, kilimo, hifadhi ya mazingira na uhifadhi wa vyanzo vya maji," alisema Kamoga. Mbunge wa jimbo la Mbulu Vijijini, Flatei Massay alipongeza kupitishwa kwa bajeti hiyo ambayo imekidhi kuondoa changamoto mbalimbali. 

Massay alisema bajeti hiyo imegusa sekta mbalimbali ikiwemo elimu ya msingi, sekondari, kilimo, mifugo, ushirika, umwagiliaji, afya na maji. Alisema anatarajia wananchi wa jimbo hilo watapiga hatua kubwa ya maendeleo kupitia utekelezaji wa miradi ya mpango wa bajeti iliyopishwa na madiwani wa halmashauri ya wilaya hiyo. 

Mwanasheria wa halmashauri hiyo, Honoratus Mulokozi alisema bajeti hiyo kabla ya kupitishwa imezingatia sheria namba 9 ya serikali za mitaa ya mwaka 1982.Mulokozi alisema sheria hiyo ilifanyiwa marekebisho Januari mosi mwaka 2000 inayotaka kufuata sheria, kanuni na taratibu, wakati wa kuandaa bajeti. 
 Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Mkoani Manyara, Hudson Kamoga akizungumza baada ya Baraza la Madiwani wa Halmashauri hiyo kupitisha mpango wa bajeti ya shilingi bilioni 43.983 za mwaka wa fedha wa 2018/2019. 
 Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Mkoani Manyara, Hudson Kamoga akielezea vipaumbele vya mpango wa bajeti ya Halmashauri hiyo. 
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Mkoani Manyara, Joseph Mandoo akizungumza kwenye kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri hiyo baada ya kupitisha mpango wa bajeti ya shilingi bilioni 43.983 za mwaka wa fedha wa 2018/2019. 


Hivyo makala MBULU YAPITISHA MPANGO WA BAJETI YA MABILIONI KUKAMILISHA VIPAUMBELE VYAKE

yaani makala yote MBULU YAPITISHA MPANGO WA BAJETI YA MABILIONI KUKAMILISHA VIPAUMBELE VYAKE Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MBULU YAPITISHA MPANGO WA BAJETI YA MABILIONI KUKAMILISHA VIPAUMBELE VYAKE mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/01/mbulu-yapitisha-mpango-wa-bajeti-ya.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "MBULU YAPITISHA MPANGO WA BAJETI YA MABILIONI KUKAMILISHA VIPAUMBELE VYAKE"

Post a Comment

Loading...