Loading...

JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI LATOA ONYO KALI KUHUSU UNUNUZI WA VIFAA VYA ZIMAMOTO

Loading...
JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI LATOA ONYO KALI KUHUSU UNUNUZI WA VIFAA VYA ZIMAMOTO - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI LATOA ONYO KALI KUHUSU UNUNUZI WA VIFAA VYA ZIMAMOTO, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI LATOA ONYO KALI KUHUSU UNUNUZI WA VIFAA VYA ZIMAMOTO
link : JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI LATOA ONYO KALI KUHUSU UNUNUZI WA VIFAA VYA ZIMAMOTO

soma pia


JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI LATOA ONYO KALI KUHUSU UNUNUZI WA VIFAA VYA ZIMAMOTO

Jeshi la Zimamoto na Uokoaji limeundwa na linatekeleza majukumu yake chini ya Sheria ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji namba 14 ya mwaka 2007 (Fire and Rescue Force Act No. 14 of 2007). Majukumu makubwa ya Jeshi hili ni kuokoa Maisha na Mali katika majanga yatokanayo na moto, mafuriko, tetemeko la ardhi, ajali za barabarani pamoja na majanga mengine.
Sambamba na majukumu hayo Jeshi la Zimamoto na Uokoaji linafanya ukaguzi kwenye vyombo vya usafiri na usafirishaji, na kutoa ushauri uwekaji wa vifaa vya kinga na tahadhari. Ukaguzi huu unafanyika kwa mujibu wa sheria namba 14 ya mwaka 2007 ikisomwa pamoja na kanuni ya Vyeti na Usalama wa moto Mwaka 2008 na marekebisho  ya mwaka 2014 (Fire and Rescue Force Safety Inspections and Certificates Regulations of 2008 GN.106 and its Amendment GN 63 of 2014.) Pamoja na kanuni ya tahadhari dhidi ya moto kwenye majengo ya mwaka 2015 (Fire and Rescue Force Fire Safety Precaution in Building Regulations of 2015 GN 516.)
Kwa kuzingatia majukumu hayo Jeshi la Zimamoto na Uokoaji linajulisha umma kuwa, halifanyi biashara ya kuuza vifaa vya kuzimia moto wala kuvifanyia matengenezo (service) vifaa hivyo pamoja na mifumo ya kinga na tahadhari dhidi ya moto. Bali Jeshi la Zimamoto na Uokoaji linasimamia na kuhakiki ufungwaji wa vifaa hivyo.
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji linatoa rai kwa wamiliki wa majengo na vyombo vya usafiri na usafirishaji, wafanyabiashara na wananchi wote kuhakikisha wananunua au kufanyia matengenezo (service) vifaa na mifumo ya kinga na tahadhari dhidi ya moto kwa Mawakala waliosajiliwa kuuza vifaa vya Zimamoto (Fire Dealers) kwa mujibu wa sheria ya Jeshi.
Imetolewa na;
Ofisi ya Habari na Elimu kwa Umma
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji

03 Januari, 2018


Hivyo makala JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI LATOA ONYO KALI KUHUSU UNUNUZI WA VIFAA VYA ZIMAMOTO

yaani makala yote JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI LATOA ONYO KALI KUHUSU UNUNUZI WA VIFAA VYA ZIMAMOTO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI LATOA ONYO KALI KUHUSU UNUNUZI WA VIFAA VYA ZIMAMOTO mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/01/jeshi-la-zimamoto-na-uokoaji-latoa-onyo_3.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI LATOA ONYO KALI KUHUSU UNUNUZI WA VIFAA VYA ZIMAMOTO"

Post a Comment

Loading...