Loading...
title : KAKOLANYA KUMALIZANA NA YANGA MWISHO WA MWEZI HUU
link : KAKOLANYA KUMALIZANA NA YANGA MWISHO WA MWEZI HUU
KAKOLANYA KUMALIZANA NA YANGA MWISHO WA MWEZI HUU
Na Zainab Nyamka,Globu ya Jamii.
BAADA ya kutokuwepo katika kikosi cha Yanga kwa muda mrefu, Mlinda mlango wa timu hiyo Beno Kakolanya ameweka wazi kuwa sasa amerejea baada ya kumalizana na uongozi kuhusu stahiki zake za fedha za usajili.
Kakolanya ambaye alijiunga na Yanga msimu wa 2016/17 kutokea Tanzania Prisons ya Mbeya baada ya kufanya vizuri kwenye msimu mzuri uliopita na kusaini kandarasi ya miaka miwili.
Takribani mwezi mmoja sasa Kakolanya amekuwa nje ya kikosi cha Yanga kukiwa na taarifa kuwa ana madai yake ya fedha za usajili na kushindwa kuungana na wenzake.
Akizungumza na Globu ya Michuzi, Kakolanya amesema kuwa tayari uongozi umemuhakikishia mwishoni mwa mwezi huu watamalizana nae fedha za usajili zilizosalia ila tayari ameanza kujumuika kwenye mazoezi na wenzake.
" Uongozi umeniambia kuwa mwishoni mwa mwezi huu watanipatia stahiki zangu kwahiyo kwa sasa naendelea na mazoezi kama kawaida nikiwa tayari nimeshaungana na wenzangu toka walivyorejea kutoka Zanzibar kwenye michuano ya Mapinduzi,"amesema Kakolanya.
Awali Kakolanya aliweka shinikizo la kutokuwepo katika kikosi cha Yanga hadi hapo atakapokamilishiwa fedha zake usajili ambazo alikuwa bado hajamaliziwa na uongozi wa klabu hiyo.
Hivyo makala KAKOLANYA KUMALIZANA NA YANGA MWISHO WA MWEZI HUU
yaani makala yote KAKOLANYA KUMALIZANA NA YANGA MWISHO WA MWEZI HUU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala KAKOLANYA KUMALIZANA NA YANGA MWISHO WA MWEZI HUU mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/01/kakolanya-kumalizana-na-yanga-mwisho-wa.html
0 Response to "KAKOLANYA KUMALIZANA NA YANGA MWISHO WA MWEZI HUU"
Post a Comment