Loading...
title : DK. MAHIGA AHIMIZA MAZINGIRA MAZURI KUVUTIA WAWEKEZAJI
link : DK. MAHIGA AHIMIZA MAZINGIRA MAZURI KUVUTIA WAWEKEZAJI
DK. MAHIGA AHIMIZA MAZINGIRA MAZURI KUVUTIA WAWEKEZAJI
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Dk.Augustine Mahiga amesema kuwa ili kufikia uchumi wa viwanda ni muhimu kutengeneza mazingira mazuri ya kuwavutia wawekezaji katika sekta mbalimbali zikiwamo za sheria, kodi, ajira,vvivutio vya uwekezaji na kilimo.
Dk.Mahiga, ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam wakati anazungumza na waandishi wa habari baada ya kumaliza kuzindua kongamano la siku mbili lililoandaliwa na Ubalozi wa India nchini Tanzania kwa kushirikisha nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) pamoja na Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC).
Lengo la kongamano hilo pamoja na mambo mengine washiriki wamezungumzia namna ya ushiriki wa sasa na siku zijazo unavyoweza kuleta amani katika nchi wanachama wa jumuiya hizo.Kauli mbiu ya kongamano katika kongamano hilo inasema "Amani, utulivu na maendeleo".
Dk. Mahiga amefafanua jambo hilo si jipya kuzungumzwa isipokuwa bado halijaeleweka na hivyo linatakiwa kuzunguzwa Tanzania pamoja EAC.
“Tunamkakati madhubuti wa kujenga viwanda katika EAC na SADC. Sasa kusema nataka viwanda ni kingine, kuvuta viwanda ni kingine, kufanya viwanda vizalishe na vistawi ni jambo lingine.
"Na ukisema unataka viwanda mazingira yapo? unataka kufanikisha viwanda je utaalam upo? hapo sasa kupitia mambo hayo matatu unaweza kuendesha viwanda,” amesema Dk.Mahiga.
Waziri Mkuu Mstaafu, Dk. Salim Ahmed Salim akizungumza leo jijini Dar es Salaam kwenye Kongamano la siku mbili lililoandaliwa na Ubalozi wa India nchini Tanzania kwa kushirikisha nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) pamoja na Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC).
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Dk.Augustine Mahiga akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati akifungua rasmi Kongamano la siku mbili ambalo limeandaliwa na Ubalozi wa India nchini Tanzania.Kauli mbiu ya kongamano hilo ni Amani, Utulivu na Maendeleo.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala DK. MAHIGA AHIMIZA MAZINGIRA MAZURI KUVUTIA WAWEKEZAJI
yaani makala yote DK. MAHIGA AHIMIZA MAZINGIRA MAZURI KUVUTIA WAWEKEZAJI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala DK. MAHIGA AHIMIZA MAZINGIRA MAZURI KUVUTIA WAWEKEZAJI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/01/dk-mahiga-ahimiza-mazingira-mazuri.html
0 Response to "DK. MAHIGA AHIMIZA MAZINGIRA MAZURI KUVUTIA WAWEKEZAJI"
Post a Comment