Loading...
title : Kamishna wa Maadili awataka viongozi kutoa ushirikiano wakitakiwa kuwasilisha benk statement.
link : Kamishna wa Maadili awataka viongozi kutoa ushirikiano wakitakiwa kuwasilisha benk statement.
Kamishna wa Maadili awataka viongozi kutoa ushirikiano wakitakiwa kuwasilisha benk statement.
Kamishna wa Maadili wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Jaji (Mst) Harold Nsekela amewataka viongozi wa umma kutoa ushirikiano kwa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi pindi watakapotakiwa kuwasilisha pamoja na nyaraka nyingine “bank statement zao” kama sehemu ya tamko la raslimali na madeni.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Alhamisi January 11, 2018 ofisini kwake jijini Dar es Salaam, Kamishna Nsekela amesema Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma Na 13 ya mwaka 1995 inampa mamlaka ya kumuagiza kiongozi kuwasilisha nyaraka za mali anazomiliki zikiwemo hati za mashamba, viwanja, kadi za magali na benk statement kama sehemu ya tamko la raslimali na madeni ya kiongozi.
“Nikiwaandikia barua viongozi kuwataka kuwasilisha benk statement na nyaraka nyingine za mali wanazomiliki watoe ushirikiano kwasababu ni matakwa ya kisheria,” amesema.
Kamishn Nsekela ameeleza kuwa baada ya zoezi la kupokea tamko kukamilika tarehe 31 Desemba, 2017, zoezi linaloendelea kwa sasa ni kuchambua matamko hayo ili kuona ni viongozi wapi wataanza kuhakikiwa mali zao.
“Tukifikia wakati wa kuhakiki mali za viongozi baada ya uchambuzi wa matamko yao, watatakiwa kutoa ushirikiano. Tutataka wathibitishe mali hizo walizipataje?,” amesema na kuongeza kuwa viongozi hawatakiwi kuwa na hofu pindi wanapotakiwa kuhakikiwa mali zao kwasababu sheria ya maadili haiwazuii kumiliki mali, isipokuwa wathibitishe walivyozipata.
Kwa mujibu wa Kamhsina Nsekela, Sekretarieti ya Maadili haipokei tamko kuwatunzia viongozi bila kulifanyia kazi ndio maana lazima zoezi la uhakiki lifanyike.
“Hatupokei matamko ya viongozi kuwatunzia, lazima tuthibitishe waliyoandika ndani vinginevyo hatuna sababu ya kuwepo,” amesema.
“Viongozi wa Umma lazima waelewe kuwa tukienda kuhakiki mali zao, lengo ni kutaka kuthibitisha mali walizonazo nan ni jukumu letu kufanya hivyo sio kuwatuhumu.”
Kamishna wa Maadili wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Jaji (Mst.) Harold Nsekela akiongea na waandishi wa habari kuhusu mali zinazotakiwa kutangazwa na viongozi wa Umma katika tamko lao. Ufafanuzi huo umetolewa leo tarehe 11/1/2018 katika ofisi za Sekretarieti ya Maadili jijini Dar es Salaam.
Kamishna wa Maadili wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Jaji (Mst.) Harold Nsekela akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari waliofika ofisini kwake tarehe 11 Januari, 2018 kutaka ufafanuzi kuhusu matakwa ya kisheria ya kuwataka viongozi wa umma kuwasilisha bank statement zao katika tamko la Raslimali na Madeni. Picha zote na Joseph Ishengoma.
Hivyo makala Kamishna wa Maadili awataka viongozi kutoa ushirikiano wakitakiwa kuwasilisha benk statement.
yaani makala yote Kamishna wa Maadili awataka viongozi kutoa ushirikiano wakitakiwa kuwasilisha benk statement. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Kamishna wa Maadili awataka viongozi kutoa ushirikiano wakitakiwa kuwasilisha benk statement. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/01/kamishna-wa-maadili-awataka-viongozi.html
0 Response to "Kamishna wa Maadili awataka viongozi kutoa ushirikiano wakitakiwa kuwasilisha benk statement."
Post a Comment