Loading...

KWANDIKWA: BARABARA ZA MCHEPUO KUPUNGUZA MSONGAMANO DODOMA

Loading...
KWANDIKWA: BARABARA ZA MCHEPUO KUPUNGUZA MSONGAMANO DODOMA - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa KWANDIKWA: BARABARA ZA MCHEPUO KUPUNGUZA MSONGAMANO DODOMA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : KWANDIKWA: BARABARA ZA MCHEPUO KUPUNGUZA MSONGAMANO DODOMA
link : KWANDIKWA: BARABARA ZA MCHEPUO KUPUNGUZA MSONGAMANO DODOMA

soma pia


KWANDIKWA: BARABARA ZA MCHEPUO KUPUNGUZA MSONGAMANO DODOMA

Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, amesema kuwa ujenzi wa barabara ya Mbande – Kongwa (Km 11.7) na Chimwaga – Ihumwa (Km 10) utasaidia kupunguza msongamano kwa magari yanayoingia Dodoma mjini.

Naibu Waziri huyo ameyasema hayo wakati akikagua barabara hizo na kuridhishwa na kasi ya ujenzi wake ambapo amesisitiza kwa makandarasi wanaojenga barabara hizo kuhakikisha wanamaliza kazi hizo kwa muda uliopangwa na kwa viwango vilivyo kwenye mkataba.

“Tutaendelea kujenga na kuboresha barabara hizi za mchepuo lengo ni kupunguza foleni katikati ya mji kwani Dodoma sasa inakua kutokana na uwepo wa watumishi wengi wa Serikali na ongezeko la magari, kwa hiyo sisi kama Serikali hatuna budi kuangalia namna ya kuboresha miundombinu yetu ili ikidhi haja ya ongezeko hili”, amesema Naibu Waziri Kwandikwa.

Aidha, amefafanua kuwa barabara hizo zikikamilika zitakuwa ni njia mbadala kwa watumiaji kwani sio lazima kwa magari yote kupita mjini na badala yake yatatumia njia nyingine za mchepuo kuendelea na safari zake.

Katika hatua nyingine, Naibu Waziri Kwandikwa amekagua athari za mvua katika barabara za mji wa Dodoma na kuwataka wananchi na madereva kuchukua tahadhari ili kuepusha hatari zinazoweza kuwakabili wakati wakivuka ama kupitisha magari yao katika kipindi hiki ambacho baadhi ya sehemu za barabara zinajaa maji kutokana na mvua nyingi zinazoendelea kunyesha. 
Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Dodoma, Mhandisi Leonard Chimagu, akimuonesha Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, sehemu ya ujenzi wa barabara ya mchepuo kutoka Chimwaga-Ihumwa yenye urefu wa KM 10 inayojengwa kwa kiwango cha lami kwa ajili ya kupunguza msongamano wa magari yanayoingia mkoani humo.Mhandisi Mkazi anayesimamia ujenzi wa barabara ya Chimwaga-Ihumwa KM 10 kwa kiwango cha lami, Mhandisi Nicholaus Mzeru, akitoa taarifa ya maendeleo ya mradi kwa waandishi wa habari ambapo mpaka sasa ujenzi wake umefikia asilimia 92.4 na KM 8 zimeshakamilika kujengwa, mkoani DodomaMeneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Dodoma, Mhandisi Leonard Chimagu, akimuonesha Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, athari za mvua eneo la katondo katika barabara za mji huo.Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, akiongozana na Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Dodoma, Mhandisi Leonard Chimagu, wakikagua athari za mvua eneo la Kibaigwa, katika barabara ya Dodoma-Dar es Salaam.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA


Hivyo makala KWANDIKWA: BARABARA ZA MCHEPUO KUPUNGUZA MSONGAMANO DODOMA

yaani makala yote KWANDIKWA: BARABARA ZA MCHEPUO KUPUNGUZA MSONGAMANO DODOMA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala KWANDIKWA: BARABARA ZA MCHEPUO KUPUNGUZA MSONGAMANO DODOMA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/01/kwandikwa-barabara-za-mchepuo-kupunguza.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "KWANDIKWA: BARABARA ZA MCHEPUO KUPUNGUZA MSONGAMANO DODOMA"

Post a Comment

Loading...