Loading...

MBUNGE KASULU VIJIJINI AAHIDI KUSIKILIZA KERO ZA WANANCHI

Loading...
MBUNGE KASULU VIJIJINI AAHIDI KUSIKILIZA KERO ZA WANANCHI - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MBUNGE KASULU VIJIJINI AAHIDI KUSIKILIZA KERO ZA WANANCHI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MBUNGE KASULU VIJIJINI AAHIDI KUSIKILIZA KERO ZA WANANCHI
link : MBUNGE KASULU VIJIJINI AAHIDI KUSIKILIZA KERO ZA WANANCHI

soma pia


MBUNGE KASULU VIJIJINI AAHIDI KUSIKILIZA KERO ZA WANANCHI

Na Rhoda Ezekiel Kigoma.

MBUNGE wa Jimbo la Kasulu Vijijini, Agaustine Vuma ameahidi kufanya ziara ya kutembelea vijijini vyote vya jimbo hilo kwa lengo la kuangalia changamoto na kero zinazo wakabili wananchi.

Amefafanua changamoto atakazokutanazo baada ya kuwasikiliza wananchi wake, hatua itakayofuata ni kuzifikisha Serikali zitatuliwe ili waendelee kufurahia uongozi wao uliopo madarakani.

Vuma amesema hayo jana wakati akikagua miradi inayotekelezwa katika jimbo hilo ikiwemo mradi wa Kituo cha Afya cha Nyakitonto kilichotengewa Sh. milioni 500." Ambapo mpaka sasa ujenzi huo umekamilika kwa asilimia 70 mpaka sasa na fedha Ilizo tumika ni Sh.milioni 290,"amefafanua Vuma.

Amesema Serikali ya Awamu ya Tano ipo kwa ajili ya kutatua changamoto za wananchi na ndio maana Rais,Dkt.John Magufuli ameanza kuboresha sekta za afya kwa kutoa fedha katika vituo vya afya.Ameongeza lengo la fedha hizo ni kuhakikisha wananchi huduma za afya vizuri pamoja na kuwawezesha wananchi kuwa na afya njema." Tunamshukuru sana Rais wetu kwa kuendelea kuwasaidia wananchi na sisi kama wawakilishi kazi yetu ni kuibua matatizo na kumpelekea aweze kuyatatua.

"Mpaka sasa tunaendelea kuboresha huduma za afya na nimeahidiwa kupewa fedha nyingine kwaajili ya kituo cha afya Rusesa na fedha hizo zitaendelea kutolewa kwa kuwa ni utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi(CCM)", amesema Vuma.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu Vijijini ambae pia ni Diwani wa kata ya Nyakitonto , Yohana Mshita amesema wananchi wa vijiji vilivyo karibu na kata hiyo walikuwa wakiteseka kupata huduma.Amesema wananchi wengine walikuwa wakilazimika kufuata huduma Kasulu Mjini na kusababisha kupoteza nguvu kazi lakini kwa sasa wataendelea kupata huduma karibu.

Ameongeza fedha zilizotolewa zimetumika kujenga chumba cha upasuaji, wodi za Wagonjwa, nyumba ya Mganga na chumba cha kuhifadhia maiti.Amesema mpaka sasa kuna fedha nyingi zimebaki, na wataendelea kuzihifadhi ili zitumike katika miradi mingine itakayo ibuliwa na wananchi

Nao baadhi ya wananchi, akiwamo Happynes Dastan amesema wamekuwa wakililia kupata kituo cha afya karibu kwani walikuwa wakilazimika kufuata huduma za upasuaji Wilaya ya Kasulu."Sasa tunauhakika wa kupata huduma za afya hapa hapa na kuendelea kufurahia huduma hiyo kwa karibu,"amesema. 

Amesema wanampongeza sana Rais wa Magufuli kwa kazi kubwa anayoifanya na shughuli ya kuwahudumia wananchi wanyonge kwa shida walizokuwa nazo.


 Mbunge wa Kasulu Vijijini Agaustine  Vuma akikagua miradi inayotekelezwa katika jimbo hilo ikiwemo mradi wa Kituo cha Afya cha Nyakitonto kilichotengewa Sh. milioni 500." Ambapo mpaka sasa ujenzi huo umekamilika kwa asilimia 70 
MBUNGE wa Jimbo la Kasulu Vijijini, Agaustine Vuma ameahidi kufanya ziara ya kutembelea vijijini vyote vya jimbo hilo kwa lengo la kuangalia changamoto na kero zinazo wakabili wananchi.


Hivyo makala MBUNGE KASULU VIJIJINI AAHIDI KUSIKILIZA KERO ZA WANANCHI

yaani makala yote MBUNGE KASULU VIJIJINI AAHIDI KUSIKILIZA KERO ZA WANANCHI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MBUNGE KASULU VIJIJINI AAHIDI KUSIKILIZA KERO ZA WANANCHI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/01/mbunge-kasulu-vijijini-aahidi.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "MBUNGE KASULU VIJIJINI AAHIDI KUSIKILIZA KERO ZA WANANCHI"

Post a Comment

Loading...