Loading...
title : MKANDARASI WA REA MBEYA NA SONGWE KUCHUKULIWA HATUA
link : MKANDARASI WA REA MBEYA NA SONGWE KUCHUKULIWA HATUA
MKANDARASI WA REA MBEYA NA SONGWE KUCHUKULIWA HATUA
Shirika la Umeme Tanzania limeagizwa kumchukulia hatua Mkandarasi ambaye ni kampuni ya wazawa ya JV State Grid Electrical & Technical Works Ltd aliyekuwa akitekeleza Mradi wa Umeme Vijijini Awamu ya Pili (REA II) Mikoa ya Mbeya na Songwe kwa kushindwa kukamilisha katika baadhi ya maeneo kwa mujibu wa makubaliano.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu ametoa agizo hilo Januari 5, 2018 kwenye mkutano na wananchi wa Kijiji cha Utengule Usongwe, Mbeya Vijijini alipokuwa kwenye ziara ya kukagua utekelezaji wa miradi ya Umeme Vijijini.
Mgalu alitoa agizo hilo kufuatia taarifa ya Meneja wa TANESCO Mkoa wa Mbeya, Mhandisi Benedict Bahati ambaye alimueleza kuhusu kampuni hiyo iliyokuwa ikitekeleza Miradi katika Wilaya za Mbarali, Rungwe, Kyela na Ileje kushindwa kukamilisha miradi yake kama ilivyopaswa kulingana na mkataba.
Alisema Serikali haitowafumbia macho Wakandarasi walioshindwa kukamilisha utekelezaji wa Miradi waliyokabidhiwa kwa mujibu wa makubaliano na aliliagiza Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kuhakikisha Mkandarasi huyo anapatikana na hatua za kisheria zinachukuliwa dhidi yake kwa mujibu wa makubaliano ya awali.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Utengule Usongwe, Mbeya Vijijini (hawapo pichani) alipokuwa kwenye ziara ya kukagua utekelezaji wa Miradi ya Umeme Vijijini Mkoani Mbeya.
Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Utengule Usongwe, Mbeya Vijijini wakimsikiliza Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza kwenye ziara yake ya kukagua utekelezaji wa Miradi ya Umeme Vijijini Mkoani Mbeya.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (kushoto) akimsikiliza Mbunge wa Mbeya Vijijini, Oran Njeza (kulia aliyesimama) wakati wa ziara yake ya kukagua utekelezaji wa Miradi ya Umeme Vijijini Mkoani Mbeya.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Utengule Usongwe, Mbeya Vijijini (hawapo pichani) alipokuwa kwenye ziara ya kukagua utekelezaji wa Miradi ya Umeme Vijijini Mkoani Mbeya.
Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Paul Mtinika (aliyesimama) akizungumza wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (wa tatu kushoto waliokaa) ya kukagua utekelezaji wa Miradi ya Umeme Vijijini Mkoani Mbeya.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (katikati) akiagana na Mbunge wa Mbeya Vijijini, Oran Njeza (kulia) mara baada ya kuzungumza na wananchi wa Kijiji cha Utengule Usongwe, Mbeya Vijijini wakati wa ziara yake ya kukagua utekelezaji wa Miradi ya Umeme Vijijini Mkoani Mbeya. Kushoto ni Meneja wa TANESCO Mkoa wa Mbeya, Mhandisi Benedict Bahati.
Hivyo makala MKANDARASI WA REA MBEYA NA SONGWE KUCHUKULIWA HATUA
yaani makala yote MKANDARASI WA REA MBEYA NA SONGWE KUCHUKULIWA HATUA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MKANDARASI WA REA MBEYA NA SONGWE KUCHUKULIWA HATUA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/01/mkandarasi-wa-rea-mbeya-na-songwe.html
0 Response to "MKANDARASI WA REA MBEYA NA SONGWE KUCHUKULIWA HATUA"
Post a Comment