Loading...

NAPE AFUNGUKA AKIMNADI DK. NDUMBARO ADAI KAMWE HATA IHAMA CCM

Loading...
NAPE AFUNGUKA AKIMNADI DK. NDUMBARO ADAI KAMWE HATA IHAMA CCM - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa NAPE AFUNGUKA AKIMNADI DK. NDUMBARO ADAI KAMWE HATA IHAMA CCM, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : NAPE AFUNGUKA AKIMNADI DK. NDUMBARO ADAI KAMWE HATA IHAMA CCM
link : NAPE AFUNGUKA AKIMNADI DK. NDUMBARO ADAI KAMWE HATA IHAMA CCM

soma pia


NAPE AFUNGUKA AKIMNADI DK. NDUMBARO ADAI KAMWE HATA IHAMA CCM

Na Gideon Mwakanosya-Songea

MBUNGE wa jimbo la Mtama mkoa wa Lindi Nape Nnauye amefunguka kwa kudai kuwa hawezi kukihama chama cha mapinduzi (CCM) kama baadhi ya watu wakiwemo wa vyama vya upinzani kwa kile alichodai kuwa magari ya upinzani yanaenda kuzama na hayajulikani yataibuka lini.

Uwazi huo ameuweka jana wakati akimnadi mgombea ubunge wa jimbo la Songea mjini mkoani Ruvuma kwa tiketi ya CCM Dk, Damas Ndumbaro kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya bombambili Manispaa ya Songea.

Nnauye ambaye aliwahi kuwa katibu wa hitikadi na uenezi CCM taifa na Waziri wa Habari, Michezo na Sanaa katika serikali ya awamu ya tano alisema kuwa kama kuna watu walidhani atakihama chama cha mapinduzi (CCM) na kwenda upinzani wasahau kabisa .

Akizungumza kwa kujiamini huku akishangiliwa na mamia ya wakazi wa bombambili alisema kuwa kama kuna kuwa na matatizo ndani ya CCM tunaonyana ndani ya chama na kuyamaliza na siyo kuhama chama.
“Naikubali serikali ya awamu ya tano inayongonzwa na jemedali Dk. John Magufuli pamoja na makamu wa Rais na waziri mkuu wake kuwa ipo imara na mimi naapa kufia CCM na siyo vinginevyo” alisema Nape Nnauye.

“Nasikia maneno maneno kutoka kwa baadhi ya watu wakisema Nape anataka kuhamia upinzani jambo ambalo siyo la kweli kuanzia leo watu hao waondokane na mawazo hayo” alisema mbunge wa Mtama Nape Nnauye.
Katika kampeni hizo ambazo uchaguzi wake utafanyika Januari 13 mwaka huu Nape Nnauye na Moses Machali aliyewahi kuwa mbunge wa jimbo la Kasulu mkoa wa Kigoma kwa tiketi ya NCCR Mageuzi wamekuwa kivutio kikubwa kwa wakazi wa jimbo la Songea hasa wanapokuwa majukwani.


Hivyo makala NAPE AFUNGUKA AKIMNADI DK. NDUMBARO ADAI KAMWE HATA IHAMA CCM

yaani makala yote NAPE AFUNGUKA AKIMNADI DK. NDUMBARO ADAI KAMWE HATA IHAMA CCM Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala NAPE AFUNGUKA AKIMNADI DK. NDUMBARO ADAI KAMWE HATA IHAMA CCM mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/01/nape-afunguka-akimnadi-dk-ndumbaro-adai.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "NAPE AFUNGUKA AKIMNADI DK. NDUMBARO ADAI KAMWE HATA IHAMA CCM"

Post a Comment

Loading...