Loading...
title : NIDA YAFANIKISHA SHEREHE ZA MAULID,MWINYI AWATAKA WAISLAMU KUFUATA MAAGIZO YA MTUME
link : NIDA YAFANIKISHA SHEREHE ZA MAULID,MWINYI AWATAKA WAISLAMU KUFUATA MAAGIZO YA MTUME
NIDA YAFANIKISHA SHEREHE ZA MAULID,MWINYI AWATAKA WAISLAMU KUFUATA MAAGIZO YA MTUME
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Waumini wa dini ya kiislamu Tanzania wametakiwa kufuata mafunzo na maagizo ya Mtume ili kuweza kupata dhawabu mbele za Mwenyezi Mungu.
Hayo yamesemwa na Mufti Mkuu wa Tanzania Abubakar Zuber alipokuwa katika hafla ya Maulidi iliyoandaliwa na Kiwanda cha NIDA textile Mills|(T) ltd NAMERA GROUP OF INDUSTIES. amabapo amewataka Waumini wa dini hiyo kusikiliza na kufuata maamulisho ya Mwenzi Mungu.
Amesema kufanya matendo mema ikiwa na kufanya maulid kunamfanya mwanadamu kupanda daraja kwa kile ambacho anakitoa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu.
Aidha amesema waislam wameasewa kufanya matendo mema ikiwa katika biashara kutoa katika kutafuta nafasi ya daraja kwa Mwenyezi Mungu.
Nae Shekh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum alizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi pamoja na uongozi mzima wa kiwanda cha NIDA amesema hafla hiyo inafanyika kila mwaka na kwamba katika kufanya hivi kunasaidia amani ya nchi kuendelea kupatikana kwani katika kuadhimisha Maulidi hayo wanafanya maombi hasa ya kuombea taifa.
Aidha amewashukuru uongozi wa NIDA pamoja na kuwapongeza kuweza kuaanda Maulidi hayo kwani kwa kufanya hivyo wanawakumbusha waumini pamoja na watu wa dini zote kutenda mambo yatakayoleta Dhawabu mbele za Mwenyezi Mungu.
Hafla hiyo imehudhuriwa na wageni mbalimbali Mgeni rasmi akiwa ni Mh. Rais mstaafu wa Awamu ya Pili Mzee Ali Hassan Mwinyi, alieambatana na Makamu wa Rais Mstaafu Dkt. Mohammed Gharib Bilali , Waziri Ulinzi ,Dk. Hussein Mwinyi pamoja Viongozi mbalimbali wa dini ya Kiislam.

Mufti Mkuu wa Tanzania Abubakar Zuber akizungumza na waandishi habari katika mauli iliyoandaliwa na NIDA Jijini Dar es Salaam.

"Nitoe wito kwa Waumini wa dini ya Kiislamu kufuata na kusikiliza kile anachokisema Mtume kwa sababu Mtume amefundisha mambo mbalimbali ambayo yana Maslaha kwa binadamu name ulimwengu wao hivyo yawapasa kuangalia Mtume amewafundisha nini Alisema

Shekh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum akizungumza katika maulid iliyoandaliwa na NIDA.
Mh. Rais mstaafu wa Awamu ya Pili Mzee Ali Hassan Mwinyi, pamoja na Makamu wa Rais Mstaafu Dkt. Mohammed Gharib Bilali na Viongozi mbalimbali wa dini ya Kiislam katika picha wakifurahia jambo .

Hivyo makala NIDA YAFANIKISHA SHEREHE ZA MAULID,MWINYI AWATAKA WAISLAMU KUFUATA MAAGIZO YA MTUME
yaani makala yote NIDA YAFANIKISHA SHEREHE ZA MAULID,MWINYI AWATAKA WAISLAMU KUFUATA MAAGIZO YA MTUME Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala NIDA YAFANIKISHA SHEREHE ZA MAULID,MWINYI AWATAKA WAISLAMU KUFUATA MAAGIZO YA MTUME mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/01/nida-yafanikisha-sherehe-za.html
0 Response to "NIDA YAFANIKISHA SHEREHE ZA MAULID,MWINYI AWATAKA WAISLAMU KUFUATA MAAGIZO YA MTUME"
Post a Comment