Loading...
title : OPERESHENI YA BODI YA MIKOPO YA ELIMU YA JUU YASHIKA KASI KWA WANUFAIKA WA MIKOPO
link : OPERESHENI YA BODI YA MIKOPO YA ELIMU YA JUU YASHIKA KASI KWA WANUFAIKA WA MIKOPO
OPERESHENI YA BODI YA MIKOPO YA ELIMU YA JUU YASHIKA KASI KWA WANUFAIKA WA MIKOPO
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
BODI ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HELSB) imesema kuwa kwa kipindi cha miezi mitatu ya operesheni ya kudai mikopo kwa wanufaika hao watafikiwa katika ofisi zao kutokana na tangazo waliotoa hivi karibuni.
Akizungumza na waandishi wa habari katika operesheni, Mkurugenzi Msaidizi wa Urejeshaji wa Bodi ya Mikopo, Phidelis Joseph amesema kuwa utaratibu umewekwa kwa watu kulipa bila kujalisha mtu alimeajiliwa au amejiajiri.Katika operesheni hiyo wametembelea kampuni mbili ambazo zinadawa zaidi ya milioni tisa zinazotokana na faini ya kuchelewesha mikopo.
Kampuni hizo ni Hegy Engeenering(T) Limeted pamoja na Sincro Sitewatch ambapo zinadaiwa kuchelewesha malipo katika bodi ya mikopo hali ambayo inachelewesha watu wengine wasinufaike.Kampuni ya Sincro Sitewatch inadaiwa shilingi 7.6 milioni ambazo ni faini inayotokana na kuchelewesha kulipa mikopo kwa wakati uliowekwa kisheria.
Joseph amesema katika operesheni hiyo wamekuwa na changamoto zinazotokana na baadhi ya wahusika kushindwa kutoa ushirikiano pale wanapowatembelea.Aidha amesema kuwa kwa wale ambao watashindwa kulipa fedha kwa kipindi kilichowekwa bodi itawafungulia mashitaka kwa mujibu wa sheria zilizowekwa.
Kwa upande wa Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa Hegy Engeneering (T) Limited, Benedict Mushi amesema kuwa bodi inafanya utaratibu mzuri kwa kuwa kama mamlaka ya mapato nchini (TRA) kupitia wadai wake.
Amesema kuwa fedha wanazodaiwa watalipa kwa wakati kwa kutambua umuhimu fedha hiyo katika kusomesha watanzania wenye mahitaji ya mkopo wa kuweza kupata elimu kwa maendeleo ya taifa.
Mkurugenzi Msaidizi wa Urejeshaji Mikopo wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu , Phidelis Joseph akizungumza katika kampuni ya Hegy Engeneering (T) Limited kuhusiana na urejeshaji mikopo kwa wanufaika walioajiliwa katika kampuni hiyo ikiwa ni operesheni ya bodi ya mikopo kufatilia wanufaika, jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa Hegy Engeneering (T) Limited, Benedict Mushi akizungumza na maofisa wa Bodi ya Mikopo jinsi watavyotekeleza kulipa fedha katika bodi kwa muda uliopangwa, jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Msaidizi wa Urejeshaji Mikopo wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu, Phidelis Joseph akizungumza na waandishi habari kuhusiana na operesheni katika kampuni mbili ambazo wanadai zaidi ya milioni tisa, jijini Dar es Salaam.
Hivyo makala OPERESHENI YA BODI YA MIKOPO YA ELIMU YA JUU YASHIKA KASI KWA WANUFAIKA WA MIKOPO
yaani makala yote OPERESHENI YA BODI YA MIKOPO YA ELIMU YA JUU YASHIKA KASI KWA WANUFAIKA WA MIKOPO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala OPERESHENI YA BODI YA MIKOPO YA ELIMU YA JUU YASHIKA KASI KWA WANUFAIKA WA MIKOPO mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/01/operesheni-ya-bodi-ya-mikopo-ya-elimu.html
0 Response to "OPERESHENI YA BODI YA MIKOPO YA ELIMU YA JUU YASHIKA KASI KWA WANUFAIKA WA MIKOPO"
Post a Comment