Loading...
title : RC NDIKILO AWAPA ONYO WARATIBU WA ELIMU KATA /AWATAKA KUJIKITA KWENYE AJIRA YAO ILI KUINUA TAALUMA MKOANI PWANI
link : RC NDIKILO AWAPA ONYO WARATIBU WA ELIMU KATA /AWATAKA KUJIKITA KWENYE AJIRA YAO ILI KUINUA TAALUMA MKOANI PWANI
RC NDIKILO AWAPA ONYO WARATIBU WA ELIMU KATA /AWATAKA KUJIKITA KWENYE AJIRA YAO ILI KUINUA TAALUMA MKOANI PWANI
Na Mwamvua Mwinyi,Chalinze
MKUU wa mkoa wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo,amewaasa waratibu wa elimu kata,kusimamia masuala ya elimu ili kuinua kiwango cha taaluma,na atakaebainika kwenda kinyume na majukumu yake ajihesabu amejifukuzisha kazi.
Aidha hajafurahishwa na hali ya mahudhurio ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka huu ambapo mahudhurio yapo chini ya asilimia 50 kimkoa.Pamoja na hayo,ametoa rai kukamatwa na kufikishwa mahakamani , wazazi na walezi wote ambao watashindwa kuwapeleka watoto wao kuripoti shule kwa wakati.
Ndikilo,aliyasema hayo ,wakati akizungumza na baadhi ya waratibu wa kata, maafisa elimu wa Chalinze na Bagamoyo,walimu na wajumbe wa bodi ya shule ya sekondari Mboga,iliyopo Chalinze .Alisema mratibu wa elimu kata atakayefanya uzembe na kubainika kujishughulisha na masuala tofauti na kazi yake atamvua kazi.
Ndikilo ,aliwapa siku saba kuhakikisha hali ya mahudhurio ya wanafunzi wa kidato cha kwanza mashuleni inakuwa nzuri tofauti na sasa.Alisema hali ya mahudhurio hairidhishi ,kwani wanafunzi waliotakiwa kuripoti shule ya sekondari Mboga hadi sasa ni asilimia 51 pekee.
Kaimu afisa elimu sekondari halmashauri ya Chalinze ,Irene Lubega akimkabidhi ripoti ya taarifa ya mahudhurio ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mashuleni hadi sasa ,mkuu Wa Mkoa Wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo,ambapo mahudhurio hayaridhishi kimkoa bado yakiwa chini ya asilimia 50
Kaimu afisa elimu sekondari halmashauri ya Bagamoyo ,Juma Yusuph akisoma ripoti ya taarifa ya mahudhurio ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mashuleni hadi sasa mbele ya mkuu Wa Mkoa Wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo,ambapo mahudhurio hayaridhishi kimkoa bado yakiwa chini ya asilimia 50
Mbunge wa jimbo la Chalinze ,Ridhiwani Kikwete akizungumzia masuala ya kielimu mara baada ya mkuu wa mkoa wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo ,kupitia shule ya sekondari Mboga ,Chalinze kuzungumzia hali ya mahudhurio ya wanafunzi wanaotakiwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka huu ambapo hali ya mahudhurio mashuleni hayaridhishi kimkoa bado yakiwa chini ya asilimia 50
Mkuu Wa Mkoa Wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo(aliyesimama) akizungumzia masuala ya kielimu mara baada ya kupitia shule ya sekondari Mboga ,Chalinze kuzungumzia hali ya mahudhurio ya wanafunzi wanaotakiwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka huu ambapo hali ya mahudhurio mashuleni hayaridhishi kimkoa bado yakiwa chini ya asilimia 50.Picha na Mwamvua Mwinyi
Hivyo makala RC NDIKILO AWAPA ONYO WARATIBU WA ELIMU KATA /AWATAKA KUJIKITA KWENYE AJIRA YAO ILI KUINUA TAALUMA MKOANI PWANI
yaani makala yote RC NDIKILO AWAPA ONYO WARATIBU WA ELIMU KATA /AWATAKA KUJIKITA KWENYE AJIRA YAO ILI KUINUA TAALUMA MKOANI PWANI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala RC NDIKILO AWAPA ONYO WARATIBU WA ELIMU KATA /AWATAKA KUJIKITA KWENYE AJIRA YAO ILI KUINUA TAALUMA MKOANI PWANI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/01/rc-ndikilo-awapa-onyo-waratibu-wa-elimu.html
0 Response to "RC NDIKILO AWAPA ONYO WARATIBU WA ELIMU KATA /AWATAKA KUJIKITA KWENYE AJIRA YAO ILI KUINUA TAALUMA MKOANI PWANI"
Post a Comment