Loading...
title : REPOA YAONGOZA MKUTANO WA WHY THINKS MATTER NCHINI
link : REPOA YAONGOZA MKUTANO WA WHY THINKS MATTER NCHINI
REPOA YAONGOZA MKUTANO WA WHY THINKS MATTER NCHINI
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
Tasisi ya Utafiti nchini Repoa leo imeongoza watafiti mbalimbali nchini katika Mkutano wa Watafiti Duniani ujulikanao kama "WHY THINKS MATTER" Ambao umefanywa na watafiti wote Duniani kuanzia Saa tatu mpaka Saa tano.
Dr Mmari amesema kuwa Mkutano huo unafanyika na nchi 170 Duniani amabpo mwaka huu wanazungumzia Umuhimu wa Tasisi za Utafiti wa Duniani ambapo kwa sasa kumekuwa na Changamoto ya ukuwaji wa teknolojia na watu kupotosha tafiti kutoka na hali ya kisiasa.
"siku hizi kuna changamoto ya mitandao ya kijamii taharifa zinasambaa haraka na taharifa zingine azina ukweli wowote na kusababisha viongozi wakaziamini na kuzitumia katika utungaji wa sera na kuendesha shughuli mbalimbali za Serikali , hivyo ikaonekana kuwa ni muhimu mwaka huu wakazungumzia tafiti ambazo zimefanyiwa kazi kisayansi" Amesema Dr Mmari.
amesema umuhimu wa Watafiti umeweza kusaidia katika kufanya Maendeleo ya kweli hivyo nashawishi Watanzania waweze kuendelea kufanya tafiti ambazo zinaweza zitatumika kwa ajili ya mipango ya Maendeleo ya Serikali na Wadau Mbalimbali.
Amemaliza kwa kusema kuwa si vyema watafaiti wakafanya tafiti ambazo zinawekwa tu kwenye makabati pasipo kuwa na Matokeo yoyote kwa Taifa.
Mkurugenzi Mkuu wa Tasisi ya Utafiti Nchini,REPOA, Dr Donald Mmari akizungumza wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa Wadau wa Tafiti Duniani ambao kwa Tanzania ulifanyika katika Ofisi za Repoa na kuitwa jina la Umuhimu wa Tafiti Duniani
Balozi wa Swideni Nchini, Katarina Rangnitt akizungumza wakati wa Mkutano wa Watafiti Duniani(WHY THINK TANKS MATTER) uliofanyika katika Taasisi ya utafiti ya Repoa kwa hapa nchini.
Mtafiti Kutoka Tasisi ya Utafiti ya Repoa, Dr Blandina Kilama akizungumza wakati wa mkutano huo wa watafiti Duniani.
Baadhi ya Maprofesa walioshiriki Mkutano huo wakiongozwa na Profesa Mwesigwa Baregu wa kwanza kulia Pichani.
Sehemu ya Wajumbe wa Mkutano huo wakisikiliza Mada Mbalimbali kutoka kwa watafiti na Wadau mbalimbali.
Hivyo makala REPOA YAONGOZA MKUTANO WA WHY THINKS MATTER NCHINI
yaani makala yote REPOA YAONGOZA MKUTANO WA WHY THINKS MATTER NCHINI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala REPOA YAONGOZA MKUTANO WA WHY THINKS MATTER NCHINI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/01/repoa-yaongoza-mkutano-wa-why-thinks.html
0 Response to "REPOA YAONGOZA MKUTANO WA WHY THINKS MATTER NCHINI"
Post a Comment