Loading...
title : WLAC YAANZA KUTOA MAFUNZO KUTOKOMEZA UKATILI WA KIJINSIA,UKEKETAJI WILAYANI IRAMBA
link : WLAC YAANZA KUTOA MAFUNZO KUTOKOMEZA UKATILI WA KIJINSIA,UKEKETAJI WILAYANI IRAMBA
WLAC YAANZA KUTOA MAFUNZO KUTOKOMEZA UKATILI WA KIJINSIA,UKEKETAJI WILAYANI IRAMBA
Na,Jumbe Ismailly IRAMBA
KITUO cha Msaada wa sheria kwa Wanawake( WLAC) kimeanza kutoa mafunzo ya kutokomeza ukatili kwa kijinsia na ukeketaji pamoja na madhara yake kwa watoto wa shule za msingi za Nguvumali,Songambele na sekondari ya Ndago wilayani Iramba,Mkoani Singida ambapo katika kipindi cha wiki moja jumla ya wanafunzi 600 kutoka katika shule za msingi na sekondari walinufaika na mafunzo hayo.
Mwanasheria kutoka Kituo cha Msaada wa sheria na Wanawake (WLAC) Abia Richard aliyasema hayo kwenye mafunzo waliyotoa kwa wananchi wa Kijiji cha Zinziligi,Tarafa ya Ndago,wilayani Iramba.
Aidha Mwanasheria huyo wa WLAC alifafanua kwamba katika kipindi hicho cha wiki moja zaidi ya watu 1000 wameshapatiwa mafunzo hayo ambayo kati ya hao wanafunzi wa darasa la tano mpaka la saba wa shule za msingi na kidato cha kwanza hadi kidato cha nne ni 600 na watu wazima ni 500.
Akizungumzia sababu za kwenda kutoa mafunzo hayo kwa wanafunzi,Abia amezitaja kuwa ni kizazi na taifa la kesho,jambo ambalo endapo wakifahamu madhara yake mapema watakapokuwa wakubwa itakuwa rahisi kuepukananavyo.Kwa mujibu wa Abia kituo cha msaada wa sheria na Wanawake na watoto kikifadhiliwa na The Foundation For Civil Society kimekuwa kikiendesha mradi wake wa kupinga ukatili wa kijinsia kwa wanawake pamoja na kuzuia vitendo vya ukeketaji kwa wanawake.
Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Zinziligi,tarafa ya Ndago,wilayani Iramba wakiwa kwenye viwanja vya mikutano ya Kijiji hicho wakipatiwa mafunzo na Kituo cha Msaada wa sharia kwa wanawake (WLAC) juu ya kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia pamoja na ukeketaji pamoja na madhara yake.
Bi Esther Kileee (aliyemshikilia mkono ni Afisa mtendaji wa kata ya Ndago) kwanza akitoa ushuhuda wa kuacha kujishughulisha na vitendo vya ukeketaji baada ya kuokoka na kwamba kabla ya kuokoka alikuwa akinufaika na shughuli hizo kwa kumpatia kipato chake na alaikuwa akiwakeketa wanawake wasiopungua 50 kwa mwezi.
Mwanasheria wa WLAC, Abia Richard akiwasilisha mada kwa wananchi wa Kijiji cha Zinziligi,Kata ya Ndago,wilayani Iramba ambapo pamoja na mambo mengine alisema katika kipindi cha wiki moja zaidi ya watu 1000 walipatiwa mafunzo na kati yao,wanafunzi ni 600 na watu wazima ni 500.
Mwanasheria wa WLAC, Abia Richard ajiteta jambo na afisa mtendaji wa kata ya Ndago, Abeli Philipo Shaluo.
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala WLAC YAANZA KUTOA MAFUNZO KUTOKOMEZA UKATILI WA KIJINSIA,UKEKETAJI WILAYANI IRAMBA
yaani makala yote WLAC YAANZA KUTOA MAFUNZO KUTOKOMEZA UKATILI WA KIJINSIA,UKEKETAJI WILAYANI IRAMBA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WLAC YAANZA KUTOA MAFUNZO KUTOKOMEZA UKATILI WA KIJINSIA,UKEKETAJI WILAYANI IRAMBA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/01/wlac-yaanza-kutoa-mafunzo-kutokomeza.html
0 Response to "WLAC YAANZA KUTOA MAFUNZO KUTOKOMEZA UKATILI WA KIJINSIA,UKEKETAJI WILAYANI IRAMBA"
Post a Comment