Loading...
title : RWEGASIRA AIAGIZA TBA KUMALIZA UJENZI NYUMBA ZA ASKARI MAGEREZA KWA WAKATI
link : RWEGASIRA AIAGIZA TBA KUMALIZA UJENZI NYUMBA ZA ASKARI MAGEREZA KWA WAKATI
RWEGASIRA AIAGIZA TBA KUMALIZA UJENZI NYUMBA ZA ASKARI MAGEREZA KWA WAKATI
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Mstaafu, Projest Rwegasira (wapili kushoto) akimsikiliza Mratibu wa Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za Askari Magereza, Mhandisi Khadija Salum, alipokua anamuonyesha Katibu Mkuu huyo maeneo mbalimbali ya ujenzi wa nyumba hizo zilizopo Ukonga, jijini Dar es Salaam. Katibu Mkuu huyo aliiagiza TBA kumaliza ujenzi huo kwa muda wa miezi mitano kuanzia sasa.
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Mstaafu, Projest Rwegasira ameiagiza Wakala wa Majengo Nchini (TBA) ambao wanajenga nyumba za askari wa Jeshi la Magereza, Ukonga jijini Dar es Salaam, kuukamilisha mradi huo ndani ya miezi mitano kama walivyoahidi.
Katibu Mkuu huyo alitoa agizo hilo, jijini Dar es Salaam jana, wakati alipokua akizungumza na Maafisa wa TBA pamoja na wa Jeshi la Magereza mara baada ya kufanya ziara ya ukaguzi wa mradi huo katika eneo zinapojengwa nyumba hizo, akiwa na lengo la kujua ujenzi ulipofikia mpaka sasa.
“Licha ya maelezo yenu mlioyatoa jinsi mradi huu wa ujenzi unavyoendelea, nimeyasikiliza vizuri, na pi nimeona hatua ya mradi huo ulipofikia, ila fanyeni juu chini muhakikishe mradi huu unakamilika ndani ya miezi hiyo mitano mlioisema hapa nyie wenyewe, muongeze nguvu zaidi katika kuukamilisha mradi huu kwa wakati,” alisema Rwegasira.
Mradi huo una thamani ya shilingi bilioni 10 ambazo zilitolewa na Rais John Magufuli mara baada ya kufanya ziara yake Ukonga mwishoni mwa mwaka juzi na kutoa maelekezo wa ujenzi wa nyumba za makazi ya askari hao katika eneo hilo.
Aidha, kutokana na agizo alilolitoa Katibu Mkuu huyo ambaye ndio msimamizi mkuu na mwenye mradi huo na kukubaliana na TBA katika maelekezo hayo, hivyo ifikapo mwezi Juni mwaka huu, mradi huo unatarajiwa kukamilika.
Ujenzi huo ulianza rasmi mwanzoni mwa mwaka jana 2017, mara baada ya Desemba 19 mwaka juzi 2016, Mtendaji Mkuu wa TBA pamoja na Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, walikutana na kusaini mkataba wa makubaliano wa kuanza kwa ujenzi wa nyumba hizo.
Hivyo makala RWEGASIRA AIAGIZA TBA KUMALIZA UJENZI NYUMBA ZA ASKARI MAGEREZA KWA WAKATI
yaani makala yote RWEGASIRA AIAGIZA TBA KUMALIZA UJENZI NYUMBA ZA ASKARI MAGEREZA KWA WAKATI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala RWEGASIRA AIAGIZA TBA KUMALIZA UJENZI NYUMBA ZA ASKARI MAGEREZA KWA WAKATI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/01/rwegasira-aiagiza-tba-kumaliza-ujenzi.html
0 Response to "RWEGASIRA AIAGIZA TBA KUMALIZA UJENZI NYUMBA ZA ASKARI MAGEREZA KWA WAKATI"
Post a Comment