Loading...

SERIKALI HAITAMUONEA MTU HURUMA, SHERIA ITACHUKUA MKONDO WAKE-ULEGA

Loading...
SERIKALI HAITAMUONEA MTU HURUMA, SHERIA ITACHUKUA MKONDO WAKE-ULEGA - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa SERIKALI HAITAMUONEA MTU HURUMA, SHERIA ITACHUKUA MKONDO WAKE-ULEGA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : SERIKALI HAITAMUONEA MTU HURUMA, SHERIA ITACHUKUA MKONDO WAKE-ULEGA
link : SERIKALI HAITAMUONEA MTU HURUMA, SHERIA ITACHUKUA MKONDO WAKE-ULEGA

soma pia


SERIKALI HAITAMUONEA MTU HURUMA, SHERIA ITACHUKUA MKONDO WAKE-ULEGA

NAIBU Waziri wa Mifungo na Uvuvi,Abdallah Ulega ameteketeza zana haramu katika Ziwa Victoria.Baadhi ya zana hizo zipo nyavu za Makila zilizounganishwa 21710 zenye macho madogo,makokolo ya Sangara 695,Timba 690,makokoro ya dagaa 90 pamoja na Pikipiki tano zilizokuwa zikitumia katika kusafirisha Samaki haramu.

Akizungumza leo na wananchi wa Mwembeni wilayani Chato mkoani Geita, Ulega amewata kushirikiana na Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais John Magufuli kuwafichuwa waharifu hao ili wachukuliwe hatua za kisheria ikiwemo kupigwa faini au kwenda jela.''Serikali haitamuonea mtu huruma awe kiongozi au raia wa kawaida sheria itachukuwa mkondo wake.

"Nia yetu ni kuona samaki wanaongezaka ziwa Victoria na watu wavue kwa kufuata sheria ili Taifa lipate mapato pamoja na ajira kwa wananchi mbalimbali" amesema Ulega.Aidha amewaonya baadhi ya wafanyakazi wa hifadhi ya Lubondo kuacha tabia ya kupewa rushwa na wavivu haramu kwani wamekuwa wakiwaruhusu kuingia kwenye hifadhi na kuwafichia zana zao wanapomaliza kuvua na kuwapatia fedha laki mbili hadi tatu.

Amefafanua kuwa kwa sasa kuna oparesheni ya kitaifa ya kupambana na uvuvi haramu ambayo inaendelea maeneo ya Ziwa Victoria ikiwa na lengo la kuondoa uvuvi haramu na mitandao ya wafanyabiashara wa zana haramu za kuvulia ,biashara ya samaki wachanga na utoroshaji wa samaki na mazao ya yake,kwenda nje ya nchi kinyume cha sheria.

Aidha kiongozi wa oparesheni Gabriel Mageni ameongeza kuwa katika operesheni hiyo ambayo ina siku 13 baadhi ya mambo ambayo wameyabaini ni pamoja na baadhi ya viongozi wa vijiji na maofisa pamoja na madiwani wanaosimamia maeneo ya uvuvi kuwapa hifadhi raia wa kigeni wanaofanya shughuli za uvuvi wakiwa hawana kibali na kusababisha hasara Serikali ikiwemo kukosa mapato

Wakati huo huo Mkuu wa Wilaya ya Chato, Chato,Shaban Ntalambe ,amewatahadharisha watendaji ambao wanashirikiana na wavuvi haramu kuwa endapo kuna mtu akibainika na kitendo hicho Serikali itahakikisha inamchukulia hatua kupitia oparesheni hiyo hatabakia hata mtu mmoja anayejihusisha na shughuli hizo awe kiongozi mkubwa ama mtu wa kawaida.
 Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe.Abdalla  Ulega  akiteketeza nyavu haramu  zilizounganishwa zipatazo 21710 zenye macho madogo,makokolo ya Sangara 695,Timba 690,makokoro ya dagaa 90 wilayani Chato.
 Baadhi ya wananchi wakishuhudia zoezi la uteketezaji wa zana haramu za uvuvi wilayani Chato mkoani Geita.
 Naibu waziri wa Mifungo na Uvuvi Mhe.Abdallah Ulega akisisitiza jambo kwa wale ambao ni watumishi na viongozi kuacha kuendelea na tabia ya kushirikiana na wavuvi haramu.
 Mkuu  wa Wilaya Chato,Shaban Ntalambe akishiriki zowezi  la kutekeeza nyavu haramu
 Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe.Abdalla  Ulega akiwa ameambatana na  Mkuu  wa Wilaya chato,Shaban Ntalambe wakielekea katika kisiwa cha hifadhi ya Lubondo.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe.Abdalla  Ulega akizungumza na Wafanyakazi wa Hifadhi ya Lubondo juu ya kuacha kushirikiana na wavuvu haramu kwani wamekuwa wakiwaruhusu kuingia kwenye hifadhi na kuwafichia zana zao wanapomaliza kuvua.


Hivyo makala SERIKALI HAITAMUONEA MTU HURUMA, SHERIA ITACHUKUA MKONDO WAKE-ULEGA

yaani makala yote SERIKALI HAITAMUONEA MTU HURUMA, SHERIA ITACHUKUA MKONDO WAKE-ULEGA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala SERIKALI HAITAMUONEA MTU HURUMA, SHERIA ITACHUKUA MKONDO WAKE-ULEGA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/01/serikali-haitamuonea-mtu-huruma-sheria.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "SERIKALI HAITAMUONEA MTU HURUMA, SHERIA ITACHUKUA MKONDO WAKE-ULEGA"

Post a Comment

Loading...