Loading...
title : SERIKALI KUZIFIKIA KAYA ZOTE MASIKINI NCHINI
link : SERIKALI KUZIFIKIA KAYA ZOTE MASIKINI NCHINI
SERIKALI KUZIFIKIA KAYA ZOTE MASIKINI NCHINI
Serikali imepanga kuimarisha Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini ambao umo ndani ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) ili kuzifikia kaya zote masikini nchini.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapteni (Mstaafu) Mhe. George H. Mkuchika (Mb) amesema Bungeni leo wakati akijibu swali kuhusu utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini nchini.
“Serikali ipo katika hatua za mwisho za kuanza kuandaa sehemu ya pili ya TASAF Awamu ya Tatu ambayo itaendelea kwa miaka mingine mitano” Mhe. Mkuchika amesema na kuongeza Serikali inaelewa yapo maeneo yenye kaya zenye vigezo vya umasikini na uhitaji ambavyo bado havijafikiwa.
Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini ulianza mwaka 2013 na unatekelezwa katika Halmashauri 159 za Tanzania Bara, na Unguja na Pemba lakini si katika vijiji, mitaa na shehia zote.
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI,
OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA.
TAREHE 31 JANUARI, 2018.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapteni (Mstaafu) Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akijibu swali kuhusu utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini nchini Bungeni leo.
Hivyo makala SERIKALI KUZIFIKIA KAYA ZOTE MASIKINI NCHINI
yaani makala yote SERIKALI KUZIFIKIA KAYA ZOTE MASIKINI NCHINI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala SERIKALI KUZIFIKIA KAYA ZOTE MASIKINI NCHINI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/01/serikali-kuzifikia-kaya-zote-masikini.html
0 Response to "SERIKALI KUZIFIKIA KAYA ZOTE MASIKINI NCHINI"
Post a Comment