Loading...
title : SERIKALI YAIPATIA TAASISI YA MOI BILIONI 16 KUIMARISHA HUDUMA ZA AFYA KWA JAMII
link : SERIKALI YAIPATIA TAASISI YA MOI BILIONI 16 KUIMARISHA HUDUMA ZA AFYA KWA JAMII
SERIKALI YAIPATIA TAASISI YA MOI BILIONI 16 KUIMARISHA HUDUMA ZA AFYA KWA JAMII
Na WAMJWW. DSM.
Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Taasisi ya Tiba ya Mifupa, Ajali na Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI) shilingi Bilioni 16 ikiwa ni jitihada za Serikali katika kuboresha huduma zinazotolewa na taasisi hiyo kwa wananchi,
Hayo yamesemwa leo na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiwa katika ziara yake ya kukagua Ubora wa Huduma zinazotolewa kwa wananchi na taasisi hiyo.
“Serikali imewapa fedha, Bilioni 16 ya kununua vifaa vyakutumika kwenye jingo lao jipya, watafunga mashine mpya za kisasa pamoja na CT-Scan na MRI, Thieta pamoja na kufungua kitengo cha zarura jambo litalopunguza usumbufu kwa wananchi wanaohitaji huduma”, alisema Dkt. Ndugulile.
Kwa upande mwingine Dkt. Ndugulile ameahidi kuendelea kushirikiana na Taasisi hiyo katika kuhakikisha wanaiwezesha zaidi ili kuweza kufanya upasuaji mkubwa ndani ya nchi jambo litakalopunguza usumbufu kwa mwananchi mwenye kipato cha chini.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiongea na wananchi waliofika kupata huduma katika Taasisi ya Mifupa MOI, katika ziara yake ya kukagua ubora wa huduma za Afya zinazotolewa katika Taasisi hiyo.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akifuatilia idadi ya Dawa katika mfumo wa Kompyuta katika Taasisi ya Mifupa ya MOI.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akikagua utunzwaji na uhifadhi wa dawa, katika Taasisi ya Mifupa ya MOI wakati alipofanya ziara yake ya kukagua ubora wa huduma za Afya zinazotolewa katika Taasisi hiyo.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile (Wakwanza) akiteta jambo na viongozi wa Taasisi ya Mifupa ya MOI wakati alipofanya ziara yake ya kukagua ubora wa huduma za Afya zinazotolewa katika Taasisi hiyo, wakatika ni Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Dkt. Respicious Boniface.
Hivyo makala SERIKALI YAIPATIA TAASISI YA MOI BILIONI 16 KUIMARISHA HUDUMA ZA AFYA KWA JAMII
yaani makala yote SERIKALI YAIPATIA TAASISI YA MOI BILIONI 16 KUIMARISHA HUDUMA ZA AFYA KWA JAMII Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala SERIKALI YAIPATIA TAASISI YA MOI BILIONI 16 KUIMARISHA HUDUMA ZA AFYA KWA JAMII mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/01/serikali-yaipatia-taasisi-ya-moi.html
0 Response to "SERIKALI YAIPATIA TAASISI YA MOI BILIONI 16 KUIMARISHA HUDUMA ZA AFYA KWA JAMII"
Post a Comment