Loading...

TAA YARUDISHIWA KIWANJA CHA NDEGE KAHAMA

Loading...
TAA YARUDISHIWA KIWANJA CHA NDEGE KAHAMA - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa TAA YARUDISHIWA KIWANJA CHA NDEGE KAHAMA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : TAA YARUDISHIWA KIWANJA CHA NDEGE KAHAMA
link : TAA YARUDISHIWA KIWANJA CHA NDEGE KAHAMA

soma pia


TAA YARUDISHIWA KIWANJA CHA NDEGE KAHAMA

KAMPUNI ya madini ya ACACIA yenye kumiliki migodi ya dhahabu ya Buzwagi na Bulyahulu imekirudisha serikalini Kiwanja cha Ndege cha Kahama kwa ajili ya kuchochea maendeleo kwa ujumla.

Awali mwaka 2005 kiwanja hicho kilikabidhiwa kwa makabidhiano maalum kati ya serikali na iliyokuwa kampuni ya madini ya Barrick walioomba ili kurahisisha shughuli zao za migodini ikiwemo ya kutumia ndege kusafirisha wafanyakazi wao na vifaa. 

Katika makabidhiano hayo yaliyofanyika jana mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Bi. Zainab Telack na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhe. Elias Kwandikwa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard Mayongela aliiomba serikali kusaidia kurefusha barabara ya kutua na kuruka kwa ndege kutoka Km. 1.5 hadi kufikia Km 2, ili kufanikisha utuaji wa ndege kubwa ikiwemo ya Shirika la ndege la Tanzania (ATCL) aina ya Bombardier Q400. 

“Tunashukuru wenzetu wa ACACIA kwa kurudisha tena serikalini kiwanja hiki, lakini bado tunaimani tutaendeleza ushirikiano baina yetu, lakini ombi langu kwa serikali ni kuongeza urefu wa barabara ya kutua na kuruka kwa ndege ili ndege kubwa zaidi ziweze kutua ninaimani zitachochea shughuli za kilimo, biashara na madini na uchumi wananchi utaimarika zaidi,” alisema Bw. Mayongela. 
Naibu Waziri Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhe. Elias Kwandikwa (wanne kulia), Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Bi. Zainab Telack (Mwenye ushungi) na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard Mayongela (watatu kulia), jana wakikagua miundombinu ya Kiwanja cha Ndege cha Kahama kabla ya makabidhiano ya kurudishwa serikalini na Kampuni ya Madini ya ACACIA.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Bi. Zainabu Telack akihutubia wananchi waliofika kushughudia makabidhiano ya Kiwanja cha Ndege cha Kahama yaliyofanyika jana baina ya Kampuni ya Madini ya ACACIA na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA).
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard Mayongela (watatu kulia), akisaini nyaraka za makubaliano ya kurudishwa Kiwanja cha Ndege cha Kahama kwa serikali kutoka kwa Kampuni ya Madini ya ACACIA, ambapo wa pili kulia ni Meneja wa migodi ya dhahabu ya Buzwagi na Bulyahulu, Bw. Benedict Busuzu na wakwanza kulia ni Mwanasheria wa ACACIA, Bi Diana Wamuza, huku Naibu Waziri Sekta ya Ujenzi, Mhe. Elias Kwandikwa (mwenye miwani) na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Bi. Zainab Telack wakishughudia



Hivyo makala TAA YARUDISHIWA KIWANJA CHA NDEGE KAHAMA

yaani makala yote TAA YARUDISHIWA KIWANJA CHA NDEGE KAHAMA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala TAA YARUDISHIWA KIWANJA CHA NDEGE KAHAMA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/01/taa-yarudishiwa-kiwanja-cha-ndege-kahama.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "TAA YARUDISHIWA KIWANJA CHA NDEGE KAHAMA"

Post a Comment

Loading...