Loading...

TANESCO TABATA WALALAMIKIWA KUTELEKEZA NYAYA, NGUZO ZA MRADI KIFURU,

Loading...
TANESCO TABATA WALALAMIKIWA KUTELEKEZA NYAYA, NGUZO ZA MRADI KIFURU, - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa TANESCO TABATA WALALAMIKIWA KUTELEKEZA NYAYA, NGUZO ZA MRADI KIFURU,, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : TANESCO TABATA WALALAMIKIWA KUTELEKEZA NYAYA, NGUZO ZA MRADI KIFURU,
link : TANESCO TABATA WALALAMIKIWA KUTELEKEZA NYAYA, NGUZO ZA MRADI KIFURU,

soma pia


TANESCO TABATA WALALAMIKIWA KUTELEKEZA NYAYA, NGUZO ZA MRADI KIFURU,

WAKAZI wa Kata ya Kinyerezi eneo la Kifuru kwa Kinana wameulalamikia uongozi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kituo cha Tabata jijini Dar es Salaam kwa kitendo cha kutelekeza nguzo na nyaya za mradi wa umeme eneo hilo ambapo zimegeuka kero. 

Wakizungumza jana eneo hilo kwa nyakati tofauti na mwandishi wa habari hizi wakazi hao, wamesema TANESCO kituo cha Tabata walileta nguzo na nyaya tangu mwaka jana na kuziweka barabara inayoelekea King'azi (Kwa Godoro) Mtaa wa Tanganyika ambapo baada ya mvua za mwishoni mwa mwaka jana 2017 baadhi ya nguzo zilianguka na nyaya kutandaa chini jambo ambalo limekuwa kero baada ya kuziba barabara ya mtaa huo na magari kupita kwa taabu.

Mkazi wa Mtaa wa Tanganyika, Rashid Abdallah alisema mradi huo umechukua zaidi ya miaka miwili sasa huku wateja walioomba umeme eneo hilo wamekuwa wakizungushwa kwamba wasubiri mradi huo bila ya mafanikio. 

"...Tumeomba umeme muda mrefu sana tunaambiwa kusubiri mradi lakini mradi ndio kama hivyo wamekuja wamefunga nyaya baada ya mvua kunyesha zimeanguka na wamezitelekeza hapo hapo chini...tunapita kwa shida na wengine kwa hofu maana 
nyaya za umeme zipo chini kabisa si wote wapita njia hazijafungwa umeme sasa hii ni hatari," alisema Mkazi huyo wa Mtaa wa Tanganyika.

Alisema kwa sasa wamekuwa kama walinzi wa nguzo na nyaya hizo za TANESCO mtaani hapo maana wanahofia zikiibiwa huenda matumaini ya mradi huo wanaoahidiwa kila kukicha kukamilika ukatoweka kabisa. "Sasa hivi tumegeuka walinzi maana tunajitahidi haya manyaya yao (waya za TANESCO) waliotelekeza hapo chini baada ya kuanguka yasiibiwe...," alisema Abdallah.
 Gari na pikipiki zikipita kwa shida Mtaa wa Tanganyika, Kifuru Kata ya Kinyerezi jijini Dar es Salaam, eneo ambalo nyaya na nguzo za mradi wa umeme unaodaiwa kutelekezwa na TANESCO kituo cha Tabata kwa muda sasa baada ya kuangushwa na mvua za mwishoni mwa mwaka 2017.
Baadhi ya nguzo na nyaya za TANESCO Kituo cha Tabata Dar es Salaam zinazodaiwa kutelekezwa na kituo hicho kwa muda sasa baada ya kung'olewa na mvua. Wakazi wa eneo hilo wameilalamikia TANESCO kwa kushindwa kutatua kero hiyo na kukamilisha mradi.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


Hivyo makala TANESCO TABATA WALALAMIKIWA KUTELEKEZA NYAYA, NGUZO ZA MRADI KIFURU,

yaani makala yote TANESCO TABATA WALALAMIKIWA KUTELEKEZA NYAYA, NGUZO ZA MRADI KIFURU, Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala TANESCO TABATA WALALAMIKIWA KUTELEKEZA NYAYA, NGUZO ZA MRADI KIFURU, mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/01/tanesco-tabata-walalamikiwa-kutelekeza.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "TANESCO TABATA WALALAMIKIWA KUTELEKEZA NYAYA, NGUZO ZA MRADI KIFURU,"

Post a Comment

Loading...