Loading...
title : TANZANIA YAPATA TUZO KIMATAIFA
link : TANZANIA YAPATA TUZO KIMATAIFA
TANZANIA YAPATA TUZO KIMATAIFA
MWAMBA WA HABARI
Na Noel Rukanuga
Tanzania imepata tuzo ya kimataifa ya utekelezaji wa sera za mapambano dhidi ya magonjwa yasiyoambukiza pamoja na dola 5,000 kupitia taasisi za kiraia.
Kaimu Mkurugenzi magonjwa yasiyoambukiza, wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Sarah Maongezi (kushoto) akimkabidhi tuzo ya kimataifa Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya magonjwa yasiyoambukiza (TANCDA), Dk Tatizo Waane.
Tuzo hiyo ya mwaka 2017 imetolewa na Shirikisho la Kimataifa la Magonjwa yasiyoambukiza (Global NCDs Alliance) kwa kushirikiana na Falme za kiarabu za mji wa Sharja.
Kaimu Mkurugenzi Magonjwa yasiyoambukiza, Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Sarah Maongezi amesema magonjwa yasiyoambukiza husababisha asilimia 27 ya vifo vyote nchini.
"Taasisi changa ya waandishi wanaopambana na magonjwa yasiyoambukiza (TJNCDF) imefanikiwa kuchochea elimu hii, hivyo sina budi kuipongeza, "amesema.
Amesema magonjwa yasiyoambukiza kama moyo, mishipa ya damu, kisukari, saratani, pumu, figo, ini, macho, meno ni moja ya sababu za tishio la uhai wa binadamu duniani ambayo yanatokana na tabia za mienendo na ulaji mbaya.
"Magonjwa haya huwapata watu ambao hawashughulishi miili yao kwa kazi za kutoa jasho na mazoezi, wanaokula kwa wingi vyakula vya mafuta, sukari, chumvi na wanga hasa katika umri wa utu uzima zaidi ya miaka 30.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha wenye Kisukari, Profesa Andrew Swai amesema TJNCDF wanapaswa kujua wamefikia watu wangapi na wangapi wamebadilika kutokana na elimu waliyopata.
Hivyo makala TANZANIA YAPATA TUZO KIMATAIFA
yaani makala yote TANZANIA YAPATA TUZO KIMATAIFA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TANZANIA YAPATA TUZO KIMATAIFA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/01/tanzania-yapata-tuzo-kimataifa.html
0 Response to "TANZANIA YAPATA TUZO KIMATAIFA"
Post a Comment