Loading...
title : TATIZO LA MAJI MKURANGA KUWA HISTORIA- NAIBU WAZIRI ULEGA
link : TATIZO LA MAJI MKURANGA KUWA HISTORIA- NAIBU WAZIRI ULEGA
TATIZO LA MAJI MKURANGA KUWA HISTORIA- NAIBU WAZIRI ULEGA
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega amesema suala la maji Mkuranga ni tatizo la muda lakini sasa matumaini yameanza kuonekana baada ya benki ya Dunia kuleta mradi wa maji wa visima 29 utakaokuwa na thamani ya zaidi ya bilioni mbili.
Akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Mwanambaya, amesema kuwa mradi wa maji utakuwa historia kutokana na hatua zinazochukuliwa na serikali. Amesema katika ziara zake amekuwa akikutana na changamoto za maji lakini hatua zimeanza kuchukuliwa kwa kiangazi cha mwaka huu maji yatakuwa tayari.
Katika Mkutano huyo amehidi kutoa bati 100 na mifuko 100 ya saruji kwa ajili ya Ujenzi wa vyumba vya madarasa mawili ya shule ya Msingi Mwanambaya.
Naibu Waziri huyo ameiomba kamati ya kijiji kukutana na mganga Mkuu ili waweze kuipandisha dispensari hiyo kwenda kituo cha afya.
Mbali na hilo wananchi wa kijiji cha Mwanambaya wamemuomba mbunge Ulega kutatua changamoto mbalimbali ikiwemo kulipwa stahiki zao za kupitiwa na mradi wa mabomba ya gesi ya Kilwa Energy.
Sehemu ya wananchi wa mwanambaya katika Mkutano. picha ,Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Mwanambaya wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani wakati wa ziara yake ndani ya Jimbo la Mkuranga.
Hivyo makala TATIZO LA MAJI MKURANGA KUWA HISTORIA- NAIBU WAZIRI ULEGA
yaani makala yote TATIZO LA MAJI MKURANGA KUWA HISTORIA- NAIBU WAZIRI ULEGA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TATIZO LA MAJI MKURANGA KUWA HISTORIA- NAIBU WAZIRI ULEGA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/01/tatizo-la-maji-mkuranga-kuwa-historia.html
0 Response to "TATIZO LA MAJI MKURANGA KUWA HISTORIA- NAIBU WAZIRI ULEGA"
Post a Comment