Loading...

WAZIRI LUKUVI: SERIKALI IMEDHAMIRIA KUMALIZA MIGOGORO YA ARDHI

Loading...
WAZIRI LUKUVI: SERIKALI IMEDHAMIRIA KUMALIZA MIGOGORO YA ARDHI - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WAZIRI LUKUVI: SERIKALI IMEDHAMIRIA KUMALIZA MIGOGORO YA ARDHI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WAZIRI LUKUVI: SERIKALI IMEDHAMIRIA KUMALIZA MIGOGORO YA ARDHI
link : WAZIRI LUKUVI: SERIKALI IMEDHAMIRIA KUMALIZA MIGOGORO YA ARDHI

soma pia


WAZIRI LUKUVI: SERIKALI IMEDHAMIRIA KUMALIZA MIGOGORO YA ARDHI

Na Said Mwishehe, Globu ya jamii
WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amesema Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kumaliza changamoto ya migogoro ya ardhi nchini. 

Lukuvi ametoa kauli hiyo wakati anazungumza na Globu ya jamii ambapo amefafanua kuna jitihada na mikakati mbalimbali inafanya kutatua migogoro ya ardhi. 

Amesema migogoro ambayo wizara yake inatafuta ufumbuzi mingi ni ile ya kuanzia mwaka 2015 kurudi nyuma kwani tangu Serikali ya Awamu ya Tano imeingia madarakani hakuna mgogoro wa ardhi. 

"Kwa sehemu kubwa mimi na wasaidizi wangu tunakwenda vizuri katika kuhakikisha tunamaliza migogoro ya ardhi kama ambavyo dhamira ya Serikali hii inavyotaka. 

"Migogoro mingi imeshughulikiwa na hata iliyokuwepo ilitokana na kutoshughulikiwa kwa wakati.Baadhi ya watendaji hawakuwa  wakichukua hatua kwa haraka. 

"Kwa sasa wizarani wanajua nataka nini na ndio maana tunakwenda vizuri maana hatutaki kutumia muda mwingi kutafuta ufumbuzi wa mgogoro wa ardhi,"amesema Lukuvi. 

Ameongeza kwa kutambua namna ya utendaji kazi wa baadhi ya maofisa wake ndio maana anatumia mfumo wa kuita wananchi wenye matatizo ya ardhi na kisha kutafuta ufumbuzi wake tena hadharani. 

Waziri Lukuvi amesema kwa mwenendo wanaokwenda nao anaamini Serikali ya awamu ya tano itafika mahali hakutakuwa na migogoro mingi ya ardhi. 

Akizungumzia migogoro ya ardhi kwa Jiji la Dar es Salaam, Lukuvi amesema kwa siku tatu ambazo amekuwa akitatua migogoro ya ardhi kwa wale waliofika wizarani ameipatia ufumbuzi.

Amesema migogoro ya ardhi ambayo hajaishughulikia ni ile ambayo kesi zipo mahakamani kwani wizara yake haina uwezo wa kuingilia uamuzi wa mahakama. 

Alipoulizwa iwapo migogoro ya ardhi kwa Dar es Salaam ipo siku itakwisha, amejibu ana uhakika wa kuimaliza. 

"Kwa hali ilivyo itafika wakati hata tukiita watu wenye migogoro ya ardhi waje tuitatue hawatakuwepo maana tunakwenda vizuri katika kuishughulikia,"amesema.
Amefafanua kwa sasa atakuwa na ratiba katika wilaya mbalimbali ambapo atakwenda kwa ajili ya kushughulikia migogoro ya ardhi. 
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akimsikiliza mmoja wa wakazi wa Dar es Salaam aliyefika katika wizara hiyo wakati anasikiliza wenye migogoro ya ardhi jana.


Hivyo makala WAZIRI LUKUVI: SERIKALI IMEDHAMIRIA KUMALIZA MIGOGORO YA ARDHI

yaani makala yote WAZIRI LUKUVI: SERIKALI IMEDHAMIRIA KUMALIZA MIGOGORO YA ARDHI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI LUKUVI: SERIKALI IMEDHAMIRIA KUMALIZA MIGOGORO YA ARDHI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/01/waziri-lukuvi-serikali-imedhamiria.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "WAZIRI LUKUVI: SERIKALI IMEDHAMIRIA KUMALIZA MIGOGORO YA ARDHI"

Post a Comment

Loading...