Loading...
title : WIZARA YA AFYA ZANZIBAR YATILIANA SAINI MAKUBALIANO NA BOHARI YA DAWA TANZANIA
link : WIZARA YA AFYA ZANZIBAR YATILIANA SAINI MAKUBALIANO NA BOHARI YA DAWA TANZANIA
WIZARA YA AFYA ZANZIBAR YATILIANA SAINI MAKUBALIANO NA BOHARI YA DAWA TANZANIA
Na Ramadhani Ali – Maelezo .
WIZARA ya Afya Zanzibar imetiliana saini makubaliano ya ushirikiano na Bohari ya Dawa Tanzania (msd) katika masuala ya uagiziaji dawa na vifaa Tiba kutoka viwandani moja kwa moja na hatua hiyo itaiwezesha Zanzibar kupunguza gharama kubwa ya kuagiza dawa kutoka katika makampuni.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Bi. Asha Abdalla Juma alitia saini kwa upande wa Wizara hiyo na Mkurugenzi Mkuu Laurean Rugambwa Bwanakunu aliiwakilishi Bohari kuu ya Dawa Tanzania katika sherehe zilizofanyika Wizara ya Afya Zanzibari Mnazimmoja.
Akizungumza baada ya kutiliana sani Bi. Asha Abdalla alisema ushirikiano huo utaisaidi Serikali na wananchi kwa jumla kuwa na uhakika wa upatikanaji dawa na kupunguza mzigo wa kutumia gharama kubwa kuagiza dawa.Alisema hatua hiyo ni utekelezaji wa maagizo ya Serikali kuhakikisha dawa zote zinapatikana bila usumbufu katika Hospitali na vituo vya afya na kufanikisha malengo yake ya kuwapatia wananchi huduma bora za afya.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya ameshauri mashirikiano yaliyoanzishwa baina ya Bohari Kuu ya Dawa Zanzibar na Bohari Kuu ya Tanzania yawe endelevu na kuwa mfano kwa Taasisi nyengine za pande mbili za Muungano na ukanda mzima wa Afrika Mashariki.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar Bi. Asha Abdalla Juma na Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa Tanzania Laurean Lugambwa Bwanakunu wakitia saina makubaliano ya ushirikiano kati ya Wizara ya Afya Zanzibar na Bohari Kuu ya Dawa Tanzania katika sherehe zilizofanyika Wizara ya Afya Mnazimmoja Mjini Zanzibar.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Bi Asha Abdalla Juma na Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa Tanzania Laurean Lugambwa Bwanakunu wakibadilisha hati za makubaliano baada ya kutiliana saini makubaliano hy katika sherehe zilizofanyika Wizara ya Afya Mjini Zanzibar.
Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa Tanzania Laurean Lugambwa Bwanakunu akizungumza baada ya kutiliana saini makubaliano ya ushirikiano na Wizara ya Afya Zanzibar.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar Bi. Asha Abdalla Juma akitoa shukrani zake kwa Uongozi wa Bohari ya Dawa Tanzania baada ya kutiliana saini makubaliano ya ushirikiano kati yao. Picha na Abdalla Omara Maelezo - Zanzibar
Hivyo makala WIZARA YA AFYA ZANZIBAR YATILIANA SAINI MAKUBALIANO NA BOHARI YA DAWA TANZANIA
yaani makala yote WIZARA YA AFYA ZANZIBAR YATILIANA SAINI MAKUBALIANO NA BOHARI YA DAWA TANZANIA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WIZARA YA AFYA ZANZIBAR YATILIANA SAINI MAKUBALIANO NA BOHARI YA DAWA TANZANIA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/01/wizara-ya-afya-zanzibar-yatiliana-saini.html
0 Response to "WIZARA YA AFYA ZANZIBAR YATILIANA SAINI MAKUBALIANO NA BOHARI YA DAWA TANZANIA"
Post a Comment