Loading...
title : DK. KALEMANI AAGIZA MKANDARASI KUMALIZA HARAKA MRADI WA UMEME WILAYANI KISHAPU
link : DK. KALEMANI AAGIZA MKANDARASI KUMALIZA HARAKA MRADI WA UMEME WILAYANI KISHAPU
DK. KALEMANI AAGIZA MKANDARASI KUMALIZA HARAKA MRADI WA UMEME WILAYANI KISHAPU
Na Robert Hokororo, Ofisi ya Mkurugenzi
Waziri wa Nishati, Mh. Dk. Medard Kalemani Februari 15 mwaka amefanya ziara wilayani Kishapu ambapo amezindua ujenzi wa miradi ya kusambaza umeme vijijini inayosimamiwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA).
Akiwa kwenye vijiji vya Negezi na Mwamashele, Dk. Kalemani alimuagiza mkandarasi anajenga mradi huo kukamilisha kwa wakati na kuviunganisha vitongoji vyote kwa umeme bila kuruka nyumba.
Alimuagiza kufikia Aprili mwaka huu kazi ya kusambaza nishati hiyo iwe imekamilika ili wananchi wanufaike na huduma hiyo na hivyo kuweza kuutumia kwa shughuli za maendeleo.
“Mkandarasi ongeza kasi hakuna kulala kumaliza mradi huu hatutaki wananchi wakwame na tunahakikisha vijiji vyote 118 vinapata huduma ya umeme, nakuagiza ndani ya siku 40 hapa Mwamashele umeme uwe umewaka,” alisema.
Dk. Kalemani aliwataka wananchi hao kuutumia umeme huo kwa ajili ya shughuli za kiuchumi zikiwemo kuanzisha viwanda vidogo vidogo ili kujipatia kipato.
Pia aliwahimiza kuwa tayari kupokea nishati hiyo katika nyumba zao kwa kutandaza nyaya na kuwataka kuitunza miundombinu inayosambaza umeme ikiwemo, nguzo, nyaya na transifoma ili isaidie kutokatika kwa huduma hiyo.
Waziri wa Nishati, Mh. Dk. Medard Kalemani akizungumza na wananchi katika kijiji cha Negezi ambako aliwasha umeme katika taasisi ya Serikali ambako tayari mradi huo ulijengwa awamu iliyopita.
Mbunge wa Kishapu, Seleman Nchambi akizungumza katika mkutano wa hadhara wakati wa ziara ya Waziri wa Nishati kijiji cha Negezi.
Sehemu ya wananchi wakifuatilia matukio kwenye shughuli hiyo.
Sehemu ya nguzo zikiwa tayari zimewasili kijiji cha Negezi kwa ajili ya kuanza kusimikwa wakati wa ujenzi wa mradi huo vijiji mbalimbali.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala DK. KALEMANI AAGIZA MKANDARASI KUMALIZA HARAKA MRADI WA UMEME WILAYANI KISHAPU
yaani makala yote DK. KALEMANI AAGIZA MKANDARASI KUMALIZA HARAKA MRADI WA UMEME WILAYANI KISHAPU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala DK. KALEMANI AAGIZA MKANDARASI KUMALIZA HARAKA MRADI WA UMEME WILAYANI KISHAPU mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/02/dk-kalemani-aagiza-mkandarasi-kumaliza.html
0 Response to "DK. KALEMANI AAGIZA MKANDARASI KUMALIZA HARAKA MRADI WA UMEME WILAYANI KISHAPU"
Post a Comment