Loading...
title : Dkt. Kalemani afanya ziara Chato, Atoa wiki moja kwa mkandarasi kukamilisha usambazaji umeme
link : Dkt. Kalemani afanya ziara Chato, Atoa wiki moja kwa mkandarasi kukamilisha usambazaji umeme
Dkt. Kalemani afanya ziara Chato, Atoa wiki moja kwa mkandarasi kukamilisha usambazaji umeme
Na Greyson Mwase, Chato
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani leo tarehe 13 Februari, 2018 amefanya ziara katika wilaya ya Chato mkoani Geita lengo likiwa ni kukagua miradi ya usambazaji wa umeme vijijini inayosimamiwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA).
Akizungumza kwa nyakati tofauti na wananchi katika vijiji vya Iparamasa na Kalembela vilivyopo wilayani Chato mkoani Geita, Dkt. Kalemani ameitaka kampuni iliyopewa kazi ya kujenga miundombinu ya umeme katika vijiji husika, ya White City JV Guandong kukamilisha kazi iliyopewa ndani ya wiki moja katika kijiji cha Iparamasa na siku tatu katika kijiji cha Ilembela ili wananchi waanze kunufaika na huduma ya umeme wa uhakika.
“ Wananchi hawa wamechoka na adha ya kukosa huduma ya umeme kwa muda mrefu, ninatoa wiki moja kwa mkandarasi kuhakikisa kijiji cha Iparamasa kinapata umeme wa uhakika na siku tatu kwa kijiji cha Kalembela wanapatiwa huduma ya umeme kwa kuwa tayari nguzo zimefika katika vijiji husika,” alisema Dkt. Kalemani
Waziri Kalemani aliendelea kusema kuwa Serikali kupitia Wizara ya Nishati, imepanga kuhakikisha kuwa ifikapo mwaka 2025 asilimia ya 75 ya watanzania wanapata huduma ya umeme ambao ni wa uhakika na kuchangia nchi kutoka kwenye orodha ya nchi masikini na kuingia kwenye orodha ya nchi za kipato cha kati
Alisisitiza kuwa, kwa kutambua mchango wa nishati kwa ukuaji wa uchumi wa viwanda, Wizara ya Nishati imepanga mikakati ya kuhakikisha miradi ya REA inatekelezwa kwa wakati kwa kutenga fedha za kutosha, na usimamizi makini ili wananchi wote wanufaike na huduma ya umeme.
Aidha, katika hatua nyingine Dkt. Kalemani aliwataka wananchi wa vijiji husika kujiandaa na huduma ya umeme kwa kutandaza nyaya kwenye nyumba zao (wiring) au kuweka Kifaa Maalum cha Umeme Tayari (UMETA) ili waunganishwe na huduma ya umeme mapema.
Pia Waziri Kalemani aliwataka wananchi kuchangamkia fursa zitakazojitokeza mara baada ya upatikanaji wa nishati ya umeme wa uhakika kama vile uanzishwaji wa viwanda vya kusindika nafaka, mashine za kuchomea vyuma na kuondokana na umaskini.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani akielezea matumizi ya Kifaa Maalum cha Umeme Tayari (UMETA) kwa wananchi wa kijiji cha Iparamasa (hawapo pichani) wilayani Chato mkoani Geita.
Sehemu ya wananchi wa kijiji cha Kalembela kilichopo wilayani Chato mkoani Geita, wakifuatilia hotuba iliyokuwa inatolewa na Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (kulia) akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kalembela kilichopo wilayani Chato mkoani Geita.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani akitoa maelekezo kwa mkandarasi, wataalam kutoka Wizara ya Nishati na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Kalembela kilichopo wilayani Chato mkoani Geita.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (katikati) akisalimiana na mmoja wa wananchi mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa hadhara katika kijiji cha Kalembela kilichopo wilayani Chato mkoani Geita.
Hivyo makala Dkt. Kalemani afanya ziara Chato, Atoa wiki moja kwa mkandarasi kukamilisha usambazaji umeme
yaani makala yote Dkt. Kalemani afanya ziara Chato, Atoa wiki moja kwa mkandarasi kukamilisha usambazaji umeme Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Dkt. Kalemani afanya ziara Chato, Atoa wiki moja kwa mkandarasi kukamilisha usambazaji umeme mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/02/dkt-kalemani-afanya-ziara-chato-atoa.html
0 Response to "Dkt. Kalemani afanya ziara Chato, Atoa wiki moja kwa mkandarasi kukamilisha usambazaji umeme"
Post a Comment